Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kutua
mkoani Lindi kesho ambapo atazindua mradi wa kuunganisha mkoa huo na wa Mtwara
katika gridi ya Taifa
Hayo yameelezwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara,
Gelasius Byakanwa jana Mei 20 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu ujio wa Waziri Mkuu
Amesema kwa siku ya kesho, Waziri Mkuu
atazindua miradi mikubwa mitatu ukiwamo wa kuunganisha Lindi na Mtwara kwenye
gridi ya taifa
Pia Waziri Majaliwa atakagua miundombinu ya
uingizaji mafuta katika mkoa huo ambao unatarajia kuanza kupokea mafuta ya
petrol na dizeli mwezi ujao
“Atakwenda kujionea miundombinu ya uingizaji
mafuta kupitia bandari ya Mtwara, habari njema iliyopo kuanzia Juni utaanza
kupokea mafuta kupitia bandari ya Mtwara,” amesema Byakanwa
Amesema Waziri Mkuu atakwenda kwenye
uzinduzi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme Mtwara
Pia amesema miundombinu ya Bandari ya Mtwara
itakuwa na uwezo wa kupokea lita 25 milioni za mafuta lakini kwa kuanzia Juni
wataanza na lita 10 milioni
“Kampuni mbili tayari zimeshaagiza mafuta
lita 10 milioni, wafanyabiashara wengine sasa waone Mtwara kama sehemu ya fursa
na itapunguza msongamano," amesema.
Post a Comment