UPANDE
wa utetezi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa
Chadema akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe, wameomba
Mahakama kutupilia mbali mashtaka dhidi ya washtakiwa kwa kuwa
yanamapungufu, kisheria.
Maombi
hayo yamewasilishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu
Wilabard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili Peter
Kibatala.Hivyo amewasilisha mapingamizi nane ya kisheria yanayoshambulia uhalali wa hati ya mashtaka na mashtaka dhidi ya washtakiwa.
Katika
mapingamizi hayo, Kibatala amedai, kibali cha DPP kina mapungufu ya
kisheria kwa sababu haioneshi imetolewa kwa mashtaka yapi na pia hati
ya mashtaka imewataja majina washtakiwa wote bila ya kufafanua na pia
imetaja tu kifungu cha sheria ambacho washtakiwa wameshtakiwa nacho
Amedai,
hakuna kibali kilichowasilishwa mahakamani hapo kwa maana hiyo mashtaka
dhidi ya washtakiwa yamepelekwa mahakamani hapo bila ridhaa ya DPP.
Amedai Aidha
Kibatala ametoa ombi mbadala na kuomba, iwapo Mahakama itashindwa
kuifuta hati nzima ya mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao basi
iyafutilie mbali mashtaka ambayo yanamapungufu kisheria. Ikiwamo shtaka
la nne, latano, la sita na la saba.
Alidai,
maelezo ya mashtaka hayo yanawachanganya washtakiwa na hawawezi
kujitetea ipasavyo. Pia mashtaka hayo kufunguliwa kwake kunahitaji
ridhaa ya (DPP) ambayo haipo kutokana na mapungufu hayo, inaonesha
hakuna ridhaa yake.
Amebainisha
kwa kuwa mashtaka hayo tajwa kufunguliwa kwake kunahitaji ridhaa ya
DPP, lakini kuwa haipo tunaomba yafutiliwe mbali. Alidai Kibatala.Pia
alidai hati ya mashtaka inamapungufu kwa sababu shtaka la pili na la
Tatu hayana maelezo ya kutosheleza ya kuwapa washtakiwa msingi na uwezo
wa kuweza kujitetea kikamilifu katika kesi hiyo ya jinai.
Alidai,
katika shtaka la kufanya mkusanyiko bila kibali hati haijataja watu
waliotishiwa na wametajwa kwa wingi hivyo haijulikani ni washtakiwa ama
ni watu wengine.
Akiendelea
kuwasilisha maoungamizi hayo, kibatala amedai, mashtaka yanayowakabili
washtakiwa hao yamejichanganya na hayaonyeshi walipelekeaje kifo cha
Akwilina na hao majeruhi walijeruhiwa na nani na kwa kutumia nini.
Amedai,
maelezo katika hati ya mashtaka yamerundikana kiasi kwamba ni vigumu
mtu kujitetea na kwamba unapomshtaki mtu kwa kisababisha kifo ni lazima
utoe Maelezo ya kutosha kuonesha unamaanisha kitu Fulani ili mtu aweze
kujitetea.
Pia
amedai mapungufu mengine yaliyomo kwenye hati hiyo ni kuwa hayaoneshi
dhumuni la pamoja ambalo washtakiwa walikutana kulitenda hivyo
linawanyang'anya washtakiwa haki ya kujitetea.
Kibatala
alidai kuwa hati ya mashtaka inamapungufu kwa sababu vifungu
vilivyotajwa katika shtaka la Tatu, tano na saba siyo sahihi.
Alidai
katika shtaka la 10,11 na 12 yanamapungufu kisheria kwa sababu
hayaonyeshi watu waliochochewa kufanya makosa ni wakina nani
waliohudhuria mkutano, wakazi wa kinondoni ama wapiga kura bila kujali
itikadi zao.
AJIBU MAPIGO
Wakili
wa Serikali Mkuu,Paul Kadushi ameiomba Mahakama kuyatupilia mbali
mapingamizi yote hayo ya upande kwa kuwa hayana mashiko kisheria. Kuhusu
kibali cha DPP kinachoipa Mahakama ridhaa ya kusikiliza kesi,Kadushi
amedai hakuna uamuzi wowote ulioweka msingi kwamba ni lazima kiwepo na
nini ama hakipaswi kuwepo na nini.
Mbali
na Mbowe wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo Namba 112 ya 2018 ni
mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum
Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika.
Mbunge
wa Tarime mjini Esterher Matiko, Katibu wa chama hicho Dk Vicenti
Mashinji na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima
Mdee na mbunge wa bunda, Esther Bulaya.
Washtakiwa
hao wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 12 katika kesi ya jinai namba 112
ya mwaka 2018 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali
kinyume cha sheria na kuendelea kufanya mkusanyiko usio halali ama
maandamano yaliyosababisha kifo cha Akwilina.
Post a Comment