WADAU wa utalii mkoani Arusha
wamekabidhi msaada wa Vitanda 40 kumi vikiwa ni vya kujifungulia wamama
wajawazito na 30 ni vya kulalia wagonjwa wa kawaida kwenye kituo cha
afya cha Murieti jijini Arusha, ikiwa ni hatua ya kusaidia serikali
kuboresha huduma za afya nchini .
Akikabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 29.8 kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,mkurugenzi wa kampuni mbili za utalii Kibo Guides na Tanganyika Wilderness Campus ,Willy Chambulo, amesema kampuni zake zitaendelea kuchangia sekta ya afya na elimu .
Kwa upande wake meneja mahusiano wa Hotel ya kitalii ya Mount Meru, Quen Mpeku,ambao wametoa msaada wa Taulo 250 zenye thamani ya shilingi milioni 8
Amesema wametoa msaada huo
kusaidia wagonjwa watakaolazwa kwenye kituo hicho cha afya ikiwa ni
kusaidia kuboresha huduma ya afya kwenye Kituo hicho cha afya.
Akipokea msaada huo mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amesema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dakt John Magufuli, inaendelea na hatua ya kuboresha huduma ya afya nchini na Jijini Arusha.
Amesema kuwa hivi sasa jiji la Arusha linajenga hospital ya wilaya ambapo Raisi Magufuli amechangia shilingi bilioni 2,huku halmashauri ikiwa imetoa shilingi milioni 500.
Amesema kuwa pia serikali imetoa fedha za ujenzi wa hospital za
wilaya za Longido na Ngorongoro ambapo tayari zimeshatolewa shilingi
bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi huo.
Aidha amempongeza mkurugenzi wa kampuni hizo za Utalii kwa msaada
wake na kusema kuwa Chambulo,amekuwa mstari wa mbele katika kuchangia
maendeleo ya mkoa wa Arusha.
Awali mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Daktar Timoth Wanyonji, amesema vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa timu ya uendeshaji na uboreshaji wa huduma ya afya ya mkoa na jiji la Arusha,ambapo mkakati uliopo ni kuendelea na kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wakati wa kujifungua ikiwa ni hatua ya kuboresha huduma ya tiba na kinga.
Amesema vifo vya watoto na akina mama vinaendelea kupungua mwaka hadi mwaka kutokana na kuboresha huduma za afya na kinga.
Kwa upande wake mkurugenzi wa jiji
la Arusha,Athuman Kihamia,akipokea msaada huo amesema Kituo cha afya cha
Mriet ni kipya hivyo kupatikana kwa vifaa hivyo kutaboresha huduma ya
afya.
Ameongeza kuwa jengo la wagonjwa wa nje OPD limekamilika kwa asilimia 90 na bado wanaendelea kukamilisha majengo mengine ikiwemo la chumba cha kuhifadhia maiti, wadi ya kujifungulia, maabara, ambapo yapo ujenzi wake umefikia 50 asilima.
Post a Comment