Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Ziwa Manyara,Noelia Mhonga akizungumza na wanahabari ofisini kwake juu ya mkakati walionao wa kuhakikisha ziwa Manyara linaendelea kuwa na maji nyakati zote |
Mhifadhi ujirani mwema wa hifadhi ya Manyara, Ibrahim Ninga akizungumza na wanahabariwanaofuatilia kujua athari za kijamii kuzunguka eneo la ikolojia ya hifadhi ya ziwa Manyara na Tarangire |
Mkuu wa wilaya ya Karatu, Telesia Mahonga akizungumza na wanahabari juu ya mkakati wa kuzuia uharibifu unaofanywa na shughuli za binadamu katika vyanzo vya maji vinavyopeleka maji ziwa Manyara |
Mwenyekiti wa kijiji cha Kilimamoja, Israel David akizungumza na wanahabari hao |
Mwenyekiti wa kijiji cha Huduma Leonard Panga akizungumza na wanahabari hao |
Bango linaloelekeza kuingia katika hifadhi ya ziwa manyara |
Charles sylvester meneja wa chemchem foundation akizungumza na wanahabari hao |
Mkurugeni wa chemchem foundation Ricardo Toss akizungumza na wanahabari hao juu ya changamoto zinazotokana na shughuli za jamii katika maeneo hayo |
-Wahifadhi waomba ushirikiano na wizara saba kutatua tatizo
NA: ANDREA NGOBOLE, PMT
Serikali
wilaya ya Karatu, imetangaza mkakati ya kuzuia kutoendelea kujaa tope
hifadhi ya ziwa Manyara kwa kuhimiza wakulima wanaolima kando ya mito
inayopeleka maji katika ziwa hilo kuacha kilimo ambacho kina athari kwa
hifadhi hiyo,
Hatua
hiyo, imetangazwa na Serikali, ili kunusuru Hifadhi ya ziwa Manyara
ambayo ipo hatarini kupotea kutokana na sehemu kubwa kujaa tope na
hivyo, kuathiri mazalia ya ndege na wanyama pori.
Akizungumza
na waandishi wa habari ambao wanafanya uchunguzi kubaini athari za
kijamii katika eneo la ikolojia ya hifadhi ya Manyara na Tarangire, Mkuu
wa wilaya ya Karatu, Telesia Mahonga alisema,kama wasipochukuwa hatua
sasa, hifadhi ya ziwa Manyara itatoweka.
"sehemu
kubwa ya maji katika ziwa Manyara, yanatoka Karatu maeneo ya
Mbulumbulu, Kilimatembo,Bugery, Rothia na maeneo ya jirani,sasa kuna
wakulima bado wanalima kilimo ambacho kinaathiri ziwa kwani tope
zinaingia ziwani"alisema
Alisema
katika hatua za awali, tayari ofisi yake imeanza kuchukuwa hatua kwenda
vijijini kutoa elimu ya kilimo cha makinga maji,kuacha kulima kwenye
vyanzo vya maji na ambao watakaidi hatua za kisheria zitachukuliwa
ikiwepo kuwaondoa.
Akizungumzia
tatizo hilo,Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Ziwa Manyara,Noelia Mhonga
alisema bila jitihada za haraka kuchukuliwa na wizara mtambuka kunusuru
ziwa hiyo, hifadhi hiyo iliyo anzishwa mwaka 1960 itatoweka.
"ni
Vizuri Wizara ya tawala za mikoa za serikali za mitaa, wizara ya
Maendeleo ya mifugo na Uvuvi,wizara ya maji, wizara ya Nishati na
Madini, Wizara ya nchi ofisi ya makamu wa Rais Mazingira na wizara ya
Maliasili na Utalii, kushirikiana kupata suluhu juu ya hifadhi
hii"alisema
Alisema
tayari Makatibu wakuu wa wizara hizo, walitembelea hifadhi hiyo na
kujionea athari za shughuli za kijamii, ikiwepo kilimo, uvuvi, uchimbaji
madini na uvamizi wa mapito ya wanyama vinavyoathiri hifadhi hiyo.
Mhifadhi
ujirani mwema wa hifadhi ya Manyara, Ibrahim Ninga alisema hifadhi
hiyo, inazungukwa na vijiji 46 hivyo kutokana na ongezeko la shughuli za
kibinaadamu, mifugo na watu hifadhi ipo hatarini.
"tunajitahidi
kutoa elimu vijiji hadi kuelekeza kilimo cha kisasa,kuacha tabia ya
kuzuia maji kuingia mtoni, kuzuia uvamizi vyanzo vya maji na kuingiza
mifugo hifadhini lakini tatizo ni kubwa"alisema
Mwenyekiti
wa kijiji cha Kilimamoja, Israel David na Mwenyekiti wa kijiji cha
Huduma Leonard Panga, walisema tatizo la kilimo kinachoathiri ziwa
Manyara ni kubwa na kupitia sheria ndogo ndogo za vijiji
wanalishughulia.
"wananchi
wanagoma kuondoka kulima pembezoni mwa mito,tunatoa elimu lakini wengi
wagumu na tunaomba ushirikiano mkubwa na serikali"alisema David.
Post a Comment