TAASISI za fedha hasa mabenki yanakabiliwa na ushindani mkubwa
kutokana na ongezeko la huduma za kifedha kutolewa na makampuni ya simu.
Suala hilo limechangia kwa kiasi kikubwa kufungwa kwa benki tano, huku nyingine tano zikiwa chini ya uangalizi maalumu.
Ili kukabiliana na ushindani huo, Benki ya CRDB imejipanga kukabiliana na ushindani huo kwa mwaka 2018 ili kuona inapata ufanisi. Na hiyo pia ni kutokana na Serikali kutoa fursa kadhaa kwa mabenki nchini kujiendesha kwa faida.
Hayo yamesemwa leo Mei 19, 2018 na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei wakati anasoma taarifa yake kwenye Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki hiyo uliofanyika Ukumbi wa Simba (AICC) jijini Arusha.
"Kutokana na ushindani mkali kutoka taasisi zisizo za kifedha, hasa huduma za simu za mkononi na changamoto nyingine, benki nyingi ndogo zilikuwa na hali ngumu, na benki takribani tano zilifungwa na Benki Kuu, na benki nyingine tano ziliwekwa chini ya uangalizi maalumu.
"Ili kukabiliana na changamoto za ukwasi na kuongeza kasi ya ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi, Benki Kuu ilipunguza kiwango cha amana ya benki hadi kufikia asilimia nane (8) na kupunguza kiwango cha riba kwa mikopo ya benki za biashara kutoka asilimia 12 hadi tisa" alisema Dkt. Kimei.
Dkt. Kimei alisema kwa maana hiyo benki za biashara zina uwezo wa kukopa fedha hizo serikalini na wao kuweza kuwakopesha wafanya biashara na watu binafsi, hivyo kurudisha mzunguko wa fedha na shughuli za kawaida kwa wananchi.
Hivyo, Benki ya CRDB imejiwekea malengo ya kimkakati kwa mwaka 2018. Mpango mkakati huo wa miaka mitano 2018-2022, una lengo la kuifanya benki ya CRDB na kampuni zake tanzu kuongoza katika kupata faida kwa kukuza ubora wa rasilimali kupitia huduma kwa wateja.
Wateja hao ni wale binafsi, wadogo na wa kati, ikitumia huduma za kidijitali zenye ubora wa hali ya juu, huku wakiahidi kufanya mageuzi makubwa mwaka huu, katika matawi yao kwa lengo la kuongeza ufanisi na tija.
"Lengo kuu mwaka 2018 litakuwa ni kuongeza kasi ya mageuzi ya kidijitali na kupunguza kiwango cha mikopo chefuchefu (isiyo rudishwa kwa wakati) hadi asilimia nane, kuboresha wastani wa kiwango cha gharama na mapato hadi asilimia 58, na kufanya mageuzi ya uendeshaji kwenye matawi ya benki ili kuongeza tija na ufanisi" alisema Dkt. Kimei.

Mkurugenzi
Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akizungumza wakati akitoa
taarifa ya Benki kwa Wanahisa wa Benki hiyo, katika Mkutano Mkuu wa 23
wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Simba uliopo
katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha Mei
19, 2018. Katika Mkutano huo, Sehemu kubwa ya wajumbe wamemuomba
Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Dkt. Charles Kimei kuendelea kuitumikia
nafasi yake hiyo, ya kuingoza benki hiyo kwa miaka mingine mitano.
Hatua
hiyo ilifikia pindi, Dkt. Kimei alipowajulisha wanahisa hao wakati
alipokuwa akitoa hotuba ya mwenendo wa benki, kuwa kwenye mkutano mkuu
ujao, atawaaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa kuitumia Benki hiyo.
Kwenye
michango yao, baadhi ya wanahisa hao walisema hiki ni kipindi kigumu
kiuchumi hivyo CRDB inahitaji mtu mwenye uzoefu wa kutosha kukabiliana
na changamoto zilizopo. Mmoja wa wanahisa hao, Emburis Sirikwa wa Arusha
alisema endapo mkurugenzi huyo ataondoka na kuiacha benki hiyo, ndani
ya miaka miwili ya kutokuwanaye lazima ufanisi utapungua.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay akizunguza katika Mkutano
Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, unaofanyika kwenye Ukumbi wa
Simba uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini
Arusha Mei 19, 2018.
Mwenyekiti
wa Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, Abeid Mwasajone
akizungumza jambo kwa wajumbe wa Mkutano huo, unaofanyika Mei 19,
2018 kwenye Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
Wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, wakiwa kwenye
Mkutano huo, unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Simba wa Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha Mei 19, 2018.
Sehemu
ya Wanahisa wa Benki ya CRDB wakichangia mada mbalimbali zinazoendelea
kutolewa katika Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB,
unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa (AICC), jijini Arusha Mei 19, 2018.
Post a Comment