Na Mwandishi Wetu, IRINGA
WAHITIMU
wa kidato cha sita wa Sekondari ya Lugalo mkoani hapa wameiomba
Serikali kuisadia kuboresha miundombinu kwa ajili ya wanafunzi walemavu.
Katika
Risala yao kwa mgeni Rasmi wamesema pamoja na mafanikio mengi
waliyoyapata kupitia shule hiyo bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya
kukosekana kwa uzio, mfumo mbovu wa maji taka kukosekana kwa karatasi
maalum za walemavu wasioona pamoja na kutokuwa na miundombinu rafiki
kuwezesha kuwa salama katika mazingira ya shule kwa wanafunzi wenye
uhitaji maalum pamoja na uhaba wa waalimu wa Sayansi.
Akijibu
Risala ya wanafunzi hao, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma
shuleni hapo, Nayman Chavalla, kupitia kampuni inayoitwa Lugalo
Associate Company Limited wameanza kukarabati nyumba ya Mkuu wa shule
pamoja na ya Makamu wa shule na kuahidi kuwa umoja huo utaendelea
kusaidia shule hiyo endapo matokeo ya taaluma yataboreshwa.
Chavalla
ameongeza kuwa Umoja huo unayo nia ya dhati katika kusaidia kutatua
changamoto za elimu shuleni hapo na kuwataka walimu kufuta daraja sifuri
na daraja la nne katika matokeo ya kitaifa ili kuleta motisha kwa wadau
wanaochangia maendeleo ya shule.
Pia
amesema pamoja na kuwa Serikali inahamasisha Elimu Bure lakini bado
jukumu la kujibidiisha katika masomo na kuinua viwango vya ufaulu ni la
Mwanafunzi na waalimu wenyewe katika kukuza taaluma yenye viwango.
Mmoja
wa wahitimu mwenye ulemavu wa macho, Elizabeth Mwaisoba mwenye umri wa
miaka 18 amesema kuna haja kwa Serikali kuendelea kusaidia wazazi wenye
watoto wenye uhitaji maalum katika kupata elimu kwani inahitaji kipato
kikubwa katika kuwahudia wanafunzi wenye uhitaji wa ziada na kuiomba
Wizara husika kutillia mkazo suala la komputa zenye sauti ili nao waweze
kwenda sambamba na teknolojia ya sasa.
Felista
Mkesela, mwenye ualbino, amesema ipo haja ya waalimu kuona umuhimu wa
kuweka vifaa vya kukuza maandishi ya ubaoni na kuongeza muda wa ziada
kwa wanafunzi walio na ulemavu wawapo darasani, kwani kuwapa muda sawa
na wanafunzi wa kawaida kunaathiri kufanya vizuri katika masomo yao.
Mkuu wa Shule hiyo, Benjamin
Kabungo, amesema kwa sasa shule hiyo ina wanafunzi 63 wenye ulemavu
wakiwemo wasioona, albino, wenye uoni hafifu, na walemavu wa viungo na
kwamba walimu 4 wa Elimu Dumishi, awali Shule hiyo ambayo ilianzishwa
mwaka 1945 na kujulikana kama The H.H Aga Khani, pia imeanzisha ufugaji
wa viumbe wakiwemo panya weupe kwa ajili ya kufanya utafiti wa
Kisayansi.
Post a Comment