Picha mbalimbali wakati wa hafla ya makabidhianomiradi nayodhaminiwa na FCF katika wilaya ya Meatu ambapo hafla hii ilifanyika katika kijiji cha sakasaka wilayani Meatu hivi karibuni |
Mwandishi Wetu,Meatu.
Serikali imewataka wakazi wa wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu,kuendeleza
uhifadhi ili kunufaika ni miradi ya maendeleo inayotolewa na Taasisi ya
Friedkin Conservation Fund(FCF), inayofanya
kazi kwa niaba ya kampuni za Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) na
Mwiba Holdlings Limited zilizowekeza katika wilaya hiyo.
Mkuu
wa wilaya ya Meatu, Dk Joseph Chilongani,alitoa wito huo juzi, wakati
wa makabidhiano ya miradi yenye thamani ya zaidi ya sh 86 milioni
iliyofadhiwa FCF kwa vikundi na taasisi za umma wilayani Meatu mwaka
2017/18 hafla iliyofanyika katika kijiji cha Sakasaka.
Dk
Chilongani alisema, wilaya hiyo, imebahatika kuwa na rasilimali za
wanyamapori hivyo ni wajibu wa wananchi kuendelea kutunza rasilimali
hiyo kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.
"tumeshuhudia
hapa vikundi vya kuweka na kukopa(VICOBA), vikipokea miradi yao sasa
huu ni mfano mzuri kwa wananchi kuona umuhimu wa kuhifadhi mazingira na
wanyamapori" alisema.
Alisema misaada
hiyo, isaidie jamii kutambua umuhimu wa uhifadhi na hivyo,kuacha tabia
ya kuingizwa mifugo maeneo ya hifadhi, kukata miti ama kuharibu
mazingira.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii FCF,Alfred Mwakivike,alisema vikundi tisa vya VICOBA katika
wilaya hiyo, vimepewa fedha za mtaji kiasi cha sh 40.4 milioni ili
kuwezesha vikundi hivyo na wanachama kufanya shughuli za maendeleo.
"tumetoa zaidi ya milioni 15 kusaidia mradi wa afya zahanati ya Mwajidalala, ujenzi kituo cha michezo cha watoto wadogo mji mdogo wa Mwanhuzi na kusaidia mradi wa maji shule ya sekondari Mwandoya" alisema.
Meneja maendeleo ya jamii FCF Nana Grosse -Woodley alisema, licha ya misaada hiyo kwa vikundi vya VICOBA na
taasisi pia wana miradi ya kupambana na ujangili katika eneo hilo na
miradi mingine ya uhifadhi, Maji,Elimu, Afya na ufugaji nyuki.
Alisema
lengo ya FCF iliyoanzishwa mwaka 1994 ni kuisaidia Tanzania na watu
wake katika jitihada zao za uhifadhi wa mali asili ya nchi hii, kuishirikisha jamii inayoishi karibu au kuzunguka maeneo mbalimbali ya hifadhi.
Post a Comment