RAIS John Magufuli Ametekeleza ahadi yake kwa kutoa
Mifuko 300 ya Saruji iliyokabidhiwa leo na katibu tawala mkoa wa Arusha
Richard Kwitega ,ikiwa ni siku moja tangu ameahidi itakayotumika kwa
ajili ya ujenzi wa kanisa katoliki .
Rais Magufuli alitoa ahadi hiyo hapo jana April 8,mwaka
huu katika Misa ya kuwekwa wakfu askofu Isaac Amani kuwa askofu mkuu wa
kanisa hilo,iliyofanyika katika kanisa la mt,Thereza wa mtoto yesu
ambapo rais Magufuli alihudhulia.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo Kwitega amesema
anajisikia faraja kukabidhi mchango wa mh rais Magufuli ambao umeweza
kutimizwa kwa wakati kwa lengo la kutekeleza ujenzi wa kanisa hilo.
“Mhe rais ameungana na waumini wa kanisa hilo katika
kuchangia ujenzi huo na anajisikia amani kwa kushirikiana na waumini
katika kuhakikisha kuwa kanisa hilo lina malizika mapema iwezekanavyo.
Kwa upande wake Paroko wa parokia hilo Padri Paulo
Malisa ambaye alikabidhiwa mchango huo amempongeza rais Magufuli kwa
hatua ya kutekeleza ahadi yake kwa muda mfupi na kuahidi kuendelea
kumwombea ili aendelee kuwa na afya njema aendelee kuwahudumia
watanzania wengine wenye uhitaji
‘’Tunamshukuru sana rais kwa kutekeleza ahadi yake
ikiwa ni siku moja tu tangu ameahidi tunaona ni jinsi gani rais wetu
alivyokuwa wa vitendo zaidi kuliko maneno ,hata sisi tunashangaa zaidi
kupokea leo hii tulitarajia labda ingechukua Mwezi ama Miezi’’amesema
padre Malisa
Padri Malisa amesema kuwa malihiaji ya kanisa hilo bado
ni makubwa kwani hadi sasa wanahitaji zaidi michangi kwani hadi
kukamilika kwa kanisa hilo litagharimu kiasi cha shilingi bilioni 7
Naye paroko msaidizi wa parokia hiyo,Padri Festus
Mangwangi amesema kuwa kanisa hilo limeanza kujengwa tangu mwaka 2011 na
linajengwa kwa nguvu za wananchi na hadi sasa kiasi cha shilingi
bilioni 4 zimeshatumika .
Amesema kanisa hilo litakuwa na uwezo wa kupokea waumini 3000 kwa mkupuo
na litakuwa na sehemu tatu za kukaa waumini pia litakuwa na sehemu ya
kuzika Maaskofu itakayokuwa chini ya kanisa hilo,{GROUND FLOW}
Hata hivyo amesema changamoto kubwa wanayokumbana nayo
ni wachangiaji kutotekeleza kwa wakati michango yao jambo ambalo
linachangia kuchelewesha ujenzi wa kanisa hilo ambao kwa sasa umefikia
katika hatua ya kuweka paa.
Katibu tawala mkoa wa Arusha Richard Kwitega akikabidhi mifuko ya cement kwa viongozi wa kanisa katoliki Mtakatifu Theresia wa mtoto yesu kama ilivyoahidiwa na Raisi Magufuli kwa kanisa hilo |
Muonekano wa kanisa hilo kwa mbele |
Baadhi ya mifuko ya cement iliyotolewa na mheshimiwa Raisi Magufuli kwa kanisa hilo |
Paroko msaidizi wa parokia ya mtakatifu Theresia wa moto Yesu akionesha eneo la ujenzi wa kanisa hilo ambapo cement iliyotolewa na Mheshimiwa Raisi Magufuli itasaidia kumalizia eneo hilo |
Post a Comment