Watu wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi wapatao wanne wakiwa
wamevalia Makoti Meusi na silaha za Moto wamevamia kituo cha Mafuta cha
Manjis cha jijini hapa na kufanikiwa kupora kiasi cha sh, milioni mbili zikiwa ni fedha za Mauzo .
Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Yusufu Ilembo, akiongea ofisini kwake leo, tukio hilo limetokea Jana April I6, majira ya saa moja na nusu usiku Katika barabara ya Uhuru katikati ya Jiji la Arusha
Amesema kuwa majambazi hao walifika
eneo la tukio wakitembea Kwa mguu na kuwalazimisha wafanyakazi
waliokuwepo katika kituo hicho kulala chini huku wakifyatua risasi mbili
hewani na kuelekea ndani ya ofisi zinapohifadhiwa fedha.
Anasema majambazi wawili waliingia
ndani huku wawili wakibakia nje kudhibiti raia na baadaye wenzao
walitoka wakiwa na na kiasi hicho cha fedha na kufanikiwa kutokomea
kusiko julikana wakiwa wanatembea
Hata hivyo uongozi wa kituo hicho
umelalamikia hatua ya jeshi la Polisi kuchelewa kufika eneo la tukio na
hivyo kuwapa nafasi majambazi hao kupora kiulaini na kuondoka bila
kubughudhiwa.
Polisi wa doria wanadaiwa kufika baada ya nusu saa zaidi ,ya muda wa tukio na kukuta majambazi wameshatoweka eneo hilo
Kamanda Ilembo amekiri Polisi
kuchelewa kufika akijitetea yakuwa Magari ya doria yalikuwa eneo lingine
la Kwa Morombo umbali wa takribani kilometa moja toka eneo la tukio na
hivyo kuchukua muda kufika .
Hata hivyo habari tulizozipata leo za Tukio la Uporaji wa fedha Katika kituo cha Mafuta cha Puma
(Manjis) lililotekelezwa na Majambazi wapatao wanne ,wenye silaha za
moto ,Imefahamika kuwa kiasi cha zaidi ya sh,milioni 20,000 za Mauzo
ziliporwa.
Aidha wafanyakazi sita wa kituo hicho wameshikiliwa na polisi na wanahojiwa tangu jana kuhusiana na tukio hilo.
Mwendeshaji wa kituo hicho cha Mafuta,Mehboob Sajan
Akiongelea tukio hilo amesema kuwa Kwa wastani wa Mauzo yao Kwa siku ni
zaidi ya Lita 10,000 zenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.
"Mauzo yetu Kwa siku ni zaidi ya Lita 10,000 sasa
ukijumlisha na Mauzo ya Oil inaweza kuwa zaidi ya sh,milioni 20" Amesema
Sajan.
Aidha ameongeza kuwa Polisi inawashikilia wafanyakazi wao
sita waliokuwa zamu siku ya tukio lililotokea hapo juzi majira ya saa
moja usiku,April 15.
Post a Comment