Biteko ambae ni Mbunge wa Bukombe amesema sifa na utukufu ni kwa Mungu na hana cha kusema zaidi ya kumshukuru Mungu.
Akizungumza na Mwanachi leo Jumamosi kwa njia ya simu Biteko amesema kwa sasa hana cha kusema zaidi ya kushukuru na atasema zaidi baada ya kuapishwa na kupewa majukumu ya utendaji katika Wizara ya Madini.
Biteko alikuwa mwenyekiti wa kamati ya muda iliyochunguza madini ya Tanzanite na kugundua asilimia 80 ya madini yanayochimbwa nchini husafirishwa nje ya nchi kwa njia za magendo.
Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Geita wamepokea kwa furaha uteuzi huo na kusema Biteko amekua na nyota ya uongozi toka akiwa shuleni kazini na sasa bungeni.
Ahmed Mubarak Mkazi wa Nyarugusu ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Geita amesema Biteko ana sifa ya uongozi toka akiwa mwanafunzi na hata alipopewa kuongoza Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Geita alileta mabadiliko makubwa.
Mutta Robert mkazi wa mjini Geita alisema kuchaguliwa kwa dotto anaweza kutatua tatizo la maeneo ya uchimbaji kwa wachimbaji wadogo wanaotumia sururu badala ya sasa wachimbaji wadogo wanatambualiwa wale wenye uwezo wa kuwa na mashine.
Chanzo; Mwananchi
Pia alisema Ni mategemeo ya wachimbaji kuwa Dotto atakuja na suluhisho la tadsiri ya kisheria ya neno wachimbaji wadogo kwakua sheria ya madini haiwatambui wachimbaji wadogo wanaotumia jembe ,moko au sururu.
Post a Comment