Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya mkoa wa dar esa salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni ,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.
Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya mkoa
wa dar esa salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni
,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wakifuatilia kwa Umakini kikao hicho.
kikao kikiendelea.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis
James(MCC) akizungumza kwa Msisistizo wakati wa kikao cha Viongozi wa
Seneti Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Viongozi wa
Matawi yote ya Vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Dar es Salaam , kulia ni Kaimu
Katibu mkuu wa UVCCM Taifa
Shaka Hamdu Shaka na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar Es Salaam Mussa
Kilakala,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es
Salaam.
Sehemu ya Wajumbe wa Vyuo na Vyuo Vikuu wakifurahia jambo(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Cha
Mapinduzi Ndugu Kheri Denis James (MCC) leo amekutana na kufanya mazungumzo na
kamati ya Utekelezaji ya Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wajumbe wa Baraza la
Vijana (UVCCM) Wilaya ya Kinondoni kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi wa
marudio utakaofanyika tarehe 17 Februari, 2018.
Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti
amesisitiza kuwa nguvu ya Vijana wa CCM itumike vizuri katika kuhakikisha
CCM inashinda kwa kishindo Uchanguzi huo.
''Suala la ushindi wa CCM katika
uchaguzi huu wa marudio halina mjadala tutashinda kwa heshima, Amani na demokrasia vijana wa CCM tumejipanga vyema
kufanikisha hilo ngazi zote" Alisisitiza Mwenyekiti Kheri
Wakati huo amekutana na kufanya
mazungumzo na Viongozi wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam
pamoja na Viongozi wa Matawi yote ya Vyuo na Vyuo Vikuu vilivyopo Mkoa wa Dar
es Salaam. ''Tunatambua na kuthamini
mchango wa Vijana wenzetu wote katika jamii mkiwemo ninyi wa Vyuo na Vyuo Vikuu
tunawategemea sana hivyo tutaendelea kufanya kazi nanyi katika maeneo yote
katika kutimiza wajibu wetu wa msingi” Alibainisha Mwenyekiti Kheir.
Mazungumzo
hayo yamehudhuriwa na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka,
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Mussa Kilakala, Mwenyekiti wa Seneti
Mkoa wa Dar es Salaam Asha Feruzi pamoja na Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Alex
Gwantwa.
Post a Comment