Baada ya kupumzika katika kituo cha
Mandara katika siku ya kwanza ,Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Jenerali George
Waitara aliongoza Wazalendo 47 kutoka jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ),Wanahabari,Marafiki wa China na Tanzania pamoja na watumishi
kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika siku ya pili
ya kuelekea kilele cha Uhuru kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 56 ya
uhuru wa Tanzania.
Miongoni mwao alikuwepo ,Balozi Mstaafu na Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii ,Tanzania ,Charles Sanga.
Safari ya kuelekea kituo cha pili cha
mapumziko cha Horombo ili chagizwa na nyimbo mbalimbali ambazo
ziliongeza morali kwa wapandaji.
Makao makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) yaliwakilishwa vyema na Meneja wake wa Mawasiliano ,Pascal Shelutete .
Mwanahabri Vicky Kimaro aliwakilisha pia Magazeti ya serikali ya HABARI LEO.
Mwanahabari George Mbara alikiwalisha vyema kituo cha luniknga cha ITV.
Mwanahabari Jamila Omar yeye alifanya uwakilishi wa kituo cha Luninga cha Channel ten.
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) liliwakilishwa na Bertha Mwambela
Na Safari iliendelea ikiongozwa na Slogan ya "Mdogo Mdogo"
Mapumziko yalikuwepo mara baada ya kutembea sehemu yenye umbali mrefu.
Wengine walitumia mapumziko hayo kwa ajili ya kupata picha za kumbukumbu ya pamoja.
Na baadae Safari iliendelea.
Hali ya hewa katika Hifadhi ya taifa ya
Mlima Kilimanjaro haitabiliki ghafla linaweza onekana jua na muda
mchache tu mvua ikanyesha ,hivyo wapandaji hua wamejiandaa na aina
yoyote ile ya hali kama inavyoonekana hapa wakiwa katika mavazi rasmi ya
kuzuia mvua pindi walipowasili eneo la Nusu njia kwa ajili ya kupata
chakula.
Wazalendo wakatumia mapumziko ya Nusu njia kupata chakula cha mchana.
Safari ikaendelea kwa kupita katika mito mbalimbali ambayo imekuwa ikitiririsha maji kwa wingi.
Wazalendo walipita katika madaraja mbalimbali wakati wa upandaji wa mlima huo.
Wenye kuhitaji msaada walipata kwa wakati.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima
Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibook alihakikisha anaongozana na
Wazalendo hao katika safari ya kuelekea kilele cha Uhuru akiwa ndiye
mwenyeji wa ugeni huo.
Hatimaye safari iliyoanza saa 2:30 za
asubuhi katika kituo cha mapumziko cha Mandara ikahitimishwa majira ya
saa 11:00 za jioni katika kituo cha mapumziko cha Horombo kwa ajili ya
kujiandaa na safari ya kuelekea kituo cha Kibo kabla ya kuelekea kilele
cha Uhuru.
Post a Comment