PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MHE MWANJELWA AWATAKA WAJUNBE MKUTANO MKUU CCM MKOA WA MBEYA KUCHAGUA VIONGOZI MAKINI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza  na wajumbe wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CC...

 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza  na wajumbe wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya, Leo Disemba 3, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana  na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akifatilia Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akitoa salamu za wabunge wa Mkoa wa Mbeya wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.

Na Mathias Canal, Mbeya

Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Leo Disemba 3, 2017 amewasihi Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kuchagua viongozi makini, weledi, wenye nidhamu na kipawa cha uongozi.

Mhe Mwanjelwa ameyasema hayo wakati akitoa salamu za wabunge Wa Mkoa Wa Mbeya kwenye Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya.

Alisema kuwa wajumbe hao hawapaswi kuchagua viongozi kwa sababu ya kufahamiana, Urafiki, Ujamaa au Undugu badala yake wanapaswa kuchagua viongozi wenye maono na mtazamo chanya ili wawe mfano bora katika kukiimarisha na kukijenga Chama Cha Mapinduzi.

Mbele ya wajumbe hao Mhe Mwanjelwa kwa ushirikiano na wabunge wote Wa Mkoa Wa Mbeya wamempatia zawadi ya Pawatila Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi kwa ajili ya Kilimo cha kisasa ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi na ufanisi Wa uongozi wake kama Mwenyekiti katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2012-2017.

Alisema kuwa Zawadi hiyo inayogharimu fedha za kitanzania takribani Shilingi Milioni Tano ni michango ya wabunge hao kwa Mwenyekiti huyo kutokana na uhodari wake katika kuimarisha Chama katika Mkoa Wa Mbeya sambamba na kuyavunja makundi yote yaliyokuwepo wakati Wa uchaguzi Mkuu Wa mwaka 2015.

Akifungua Mkutano huo Mwenyekiti Wa CCM Mkoa Wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu Wa Mkoa Wa Lindi Mhe Godfrey Zambi alimpongeza Naibu Waziri Wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kwa kusafiri usiku wa manane kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano huo pamoja na kuwa na majukumu mengi ya kiserikali Wilayani Songea Mkoani Ruvuma.

Zambi alisema Kuwa kitendo cha Mhe Mwanjelwa kushiriki katika Mkutano huo kimeonyesha mfano bora na umakini katika kuheshimu Chama Cha Mapinduzi kinachoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.

Kwa upande wake Msimamizi Mkuu katika Mkutano huo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe Antony Peter Mavunde aliwataka wajumbe hao kuchagua viongozi wenye uwezo Wa kuwasaidia wanachama na wananchi katika kuchagiza shughuli za maendeleo.

Aidha, alisema uchaguzi huo unapaswa kufuata kanuni na taratibu za uchaguzi.

Mkutano huo utamalizika kwa kuchagua Mwenyekiti Wa CCM Mkoa Wa Mbeya na Mjumbe Wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top