Klabu ya soka ya Azam FC imetangaza kuachana na nyota wake wa kimataifa
Yahaya Mohamed kutoka nchini Ghana baada ya kushindwa kuonesha kiwango
cha kuridhisha.
Taarifa ya klabu hiyo imesema kuwa viongozi wamekaa na mchezaji huyo na
kumalizana vyema kwasababu pande zote mbili zinatambua changamoto za
mchezo wa soka kuwa kuna mazingira kugoma lakini pia falsafa kutoendana
na mchezaji.
Aidha klabu hiyo imesema itaendelea kukumbuka mchango mkubwa wa Yahaya
alioutoa kwenye timu hiyo hususani kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi
ambapo aliisadia klabu kuibuka mabingwa.
Yahaya ataondoka nchini kesho kurejea kwao Ghana. Azam FC imesema
itaanza mapema mchakato wa kumpata mrithi wa Yahaya ambaye atasajiliwa
wakati wa dirisha dogo kwa kufuata mapendekezo ya mwalimu.
Azam FC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania
bara ikiwa na alama 19 nyuma ya Simba SC ambayo pia ina alama 19
zikitofautiana kwa magoli ya kufunga na kufungwa.
Home
»
Matukio
»
michezo
» Azam FC Wagutuka...Wampiga Chini Mchezaji wa nje Baada ya Kutokuonyesha Kiwango
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment