Profesa Mkumbo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wawakilishi wa viongozi wa mamlaka 19 za maji kuhusu mipango mbalimbali ya kuboresha sekta ya maji nchini.
Amesema ahadi yake haitakwenda bure kwani mwaka 2020 Rais Magufuli ataanzia Dar es Salaam hadi Kigoma akipunga mkono tu bila kusema neno lakini kura zitakuwa za kishindo.
Katibu huyo amesema Wizara ya Maji ndiyo kila kitu kwani inawagusa wananchi wa hali ya chini na juu na ndiyo maana kuna ulazima wa kuwa na usimamizi wa kutosha.
Kutokana na hilo Profesa Kitila amekemea tabia ya vyama vya wafanyakazi kutengeneza majungu ya wivu na kugeuza mamlaka za maji kuwa vichaka vya majungu na umbea ambapo matokeo yake ni kuumiza na kuwabambikizia tuhuma viongozi wakiwemo wakurugenzi wa mamlaka hizo.
Amewataka wafanyakazi kupigania haki zao huku wakitimiza wajibu wao kwani bila wao kufanya kazi kwa tija hawawezi kuwa na haki ya kudai maslahi bora.
Katibu wa kikao hicho Robert Chilewa amesema mamlaka hizo zimekuwa na changamoto kubwa kutokana madeni yanayofikia Sh 15 bilioni kutoka taasisi na mashirika ya umma.
Amesema mamlaka zimeanza kuyumba kwa utendaji kazi kutokana na kuondolewa kwa watumishi wasiofikia elimu ya kidato cha nne ambao walikuwa nguzo imara huku Wilaya ya Wanging'ombe anakotoka Waziri wa Maji ikiwa na watumishi asilimia 72 wote wa darasa la saba na akamwomba Profesa Kitila awasaidie watumishi hao warudishwe kazini.
CHANZO: Mwananchi
Post a Comment