Waziri
wa Maliasilia na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa
ufunguzi wa mkutano wa mwaka baina ya Hifadhi za Taifa, Wahiri na
Waandishi wa aandamizi wa habari nchini, ulioanza leo jijini Tanga.
NA: ANDREA NGOBOLE PMT
Wahariri
na Wanahabari nchini wametakiwa kuhakikisha wanaendelea kutumia vyema kalamu zao katika kuandika
masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya utalii wa Tanzania ili kuutangaza ikiwa sambamba
na kuchangia kukuza uchumi wa Taifa
Wito
huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne
Maghembe wakati akifungua mkutano wa sita wa wahariri na wanahabari
waandamizi unaohusu sekta ya utalii nchini ambao umeandaliwa na Hifadhi
za Taifa (TANAPA) unaofanyika jijini Tanga mapema leo ukiwa na kauli mbiu ya Utalii na Tanzania ya Viwanda.
Waziri Maghembe amesema sekta ya habari ina mchango mkubwa katika kukuza sekta ya utalii nchini, hivyo wanahabari wanatakiwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa jamii kupitia habari na makala mbalimbali wanazoandika.
"Mchango wa vyombo vya habari ni muhimu sana katika kukuza sekta ya utalii, mmekuwa mnaandika sana lakini naomba muendelee kuandika zaidi ili tuweze kuwa na sekta ya utalii yenye ustawi mzuri," amesema.
Waziri Maghembe amesema sekta ya habari ina mchango mkubwa katika kukuza sekta ya utalii nchini, hivyo wanahabari wanatakiwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa jamii kupitia habari na makala mbalimbali wanazoandika.
"Mchango wa vyombo vya habari ni muhimu sana katika kukuza sekta ya utalii, mmekuwa mnaandika sana lakini naomba muendelee kuandika zaidi ili tuweze kuwa na sekta ya utalii yenye ustawi mzuri," amesema.
Pia amewataka wanahabari kuhakikisha wanaandika habari zenye tija kwa jamii kwani utalii umekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi na kwamba una changamoto kubwa kwani wanashindana na nchi nyingine zinazotegemea utalii kama Kenya,Uganda, Rwanda, Msumbiji na Afrika kusini
"Nyinyi
waandishi wa habari msikubali kuandika jambo ambalo hamlijui kitaaluma,
kwani ukifanya hivyo utakuwa hujengi jamii yako,hivyo ni muhimu sana
kwa wanahabari kujua habari sahihi za uhifadhi hasa kwa kuzungumza na
wataalamu kutoka sekta hiyo"amesema Prof. Maghembe.
Amesema
kwa sasa watu mbalimbali duniani wanafahamu kuhusu vivutio vilivyopo
nchini na hiyo ni kutokana na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo
nchini.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi amesema wataendelea kushirikiana na vyombo vya habari ili kuhakikisha watanzania na watu mbalimbali duniani wanavifahamu vizuri vivutio vyvutalii vya Tanzania
amesema kuwa utalii Utalii
unachangia 17.2% ya pato la Taifa na 25% ya fedha za kigeni nchini,80%
ya utalii unatokana na Hifadhi za Taifa.
Amesema
kuwa TANAPA inajitegemea kwa asilimia 100, na mchango wao kwa serikali
umeongezeka kutoka bilioni 27 mwaka 2015/16 mpaka bilioni 34 kwa mwaka
2016/17 sawa na ongezeko la bilioni saba.
"Tanzania
ina vivutio vingi vya kipekee ukilinganisha na nchi nyingine
Duniani,Mamlaka kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii nchini pamoja na
Ofisi za Balozi zetu nchi mbalimbali inajitangaza ndani na nje ya Nchi
ili kuongeza idadi ya Watalii",amesema Kijazi.
Akielezea
Uvumi wa Mlima Kilimanjaro kuwa haupo Tanzania,anasema ni ni propaganda
za ushindani wa kibiashara, lakini matumizi ya Teknolojia yamesaidia
kutoa elimu,anasema na kuongeza kuwa hivi sasa idadi kubwa ya watalii
kutoka Nje ya nchi wanaelewa Mlima huo upo Tanzania.
Akielezea
changamoto ya Ujangili,Kijazi anaeleza kuwa kwa sasa matukio ya
ujangili yamepungua kwa 80% na kwamba Mamlaka inashirikiana na Jumuia ya
Kimataifa kutokomeza Soko la bidhaa zinazotokana na ujangili.
Meneja mahusiano wa shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) Pasco Shelutete akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo hii leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi
akizngumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jijini Tanga leo.
Washiriki wa mkutano hao wakifuatilia hotuba za ufunguzi zilizokuwa zikitolewa na viongozi mbalimbali.
Mkuu
wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani, Dk James Wakibara akiwasilisha mada ya
changamoto za mifugo katika hifadhi za taifa katika mkutano huo.
Maofisa wa TANAPA wakifuatilia mada
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano huo.
Picha ya pamoja baina ya washiriki na mgeni Rasmi.
Waziri
wa Utalii na Maliasili Prof.Jumanne Maghembe akizungumza jambo
alipokuwa akifungua Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa
Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza
kufanyika leo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli
mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
Baadhi
ya Wahariri na Wanahabari waandamizi wakifuatilia yaliyaokuwa yakijiri
kwenye mkutano huo ulioanza kufanyika leo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa
jijini Tanga, ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA),ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya
Viwanda'.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shrika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Allan Kijazi akimkaribisha
mgeni rasmi Waziri wa Utalii na Maliasili Prof.Jumanne Maghembe kufungua
Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa
Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo kwenye ofisi za
Mkuu wa Mkoa jijini Tanga,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii
na Tanzania ya Viwanda'.
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga,Mh Martin Shigella akiwakaribisha wageni mbalimbali
waliofika kuhudhuria mkutano wa mwaka wa Wahariri na Wanahabari
waandamizi,uliofanyika kwenye ukumbi uliopo kwenye ofisi zake.Mkutano
huo umebeba kauli kuu ambayo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete
akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye Mkutano wa
Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na
Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo kwenye ofisi za Mkuu wa
Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na
Tanzania ya Viwanda'.
Baadhi
ya Wahariri na Wanahabari waandamizi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri
kwenye mkutano wa Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi Waandamizi
ulioanza kufanyika leo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga,
ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),ambapo kauli mbiu
ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shrika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Allan Kijazi akimkaribisha
mgeni rasmi Waziri wa Utalii na Maliasili Prof.Jumanne Maghembe kufungua
Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa
Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo kwenye ofisi za
Mkuu wa Mkoa jijini Tanga,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na
Tanzania ya Viwanda'.
Baadhi
ya Wahariri wakifuatailia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa
Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi Waandamizi ulioanza kufanyika
leo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga
Baadhi
ya Wahariri na Wanahabari waandamizi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri
kwenye mkutano wa Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi Waandamizi
ulioanza kufanyika leo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga,
ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),ambapo kauli mbiu
ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete
akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye mkutano wa
Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi Waandamizi ulioanza kufanyika
leo kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga,ambapo kauli mbiu kuu ya
mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
Mhariri
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd.Absalom Kibanda
akitoa salamu za shukurani kwa waandaji wa mkutano pia na kueleza
changamoto kadhaa zinazopaswa kurekebishwa/kufanyiwa kazi na Shirika la
Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Baadhi ya Wahariri wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Post a Comment