Meneja Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha saruji cha Rhino Tanga, William Malonza, akimuonyesha
moja ya bidhaa zizalishwazo na kiwanda hicho, Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijage, wakati wa maonyesho ya tano ya
Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako Tanga.
Mwijage ameyafungua
maonyesho hayo leo katika viwanja ya maonyesho Mwahako ambayo
yamezishirikisha mataifa mbalimbali ya Barani Afrika na Asia.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijage, akisalimiana na Afisa Masoko kiwanda cha saruji cha Rhino Tanga, Carolina Hillary wakati alipotembelea banda la maonyesho ya tano ya Kimataifa yalifunguliwa jana Tanga katika viwanja vya maonyesho Mwahako.
Waziri wa viwanda na Biashara, Chales Mwijage, akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha Saruji cha Rhino Tanga, William Malonza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika Tanga.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijaga akipata maelekezo ya namna mkonge unavyoweza kutengeneza dawa pamoja na mafuta aina mbalimbali.
Simba ni moja katika wanyama ambao wameletwa kwa ajili ya maonyesho Tanga
Wakazi wa Tanga wakiangalia Kobe ambaye ni moja ya vivutio katika maonyesho ya tano ya Kimataifa yanayofanyika Tanga.
Post a Comment