PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: FURSA ZA AJIRA ZAPELEKWA VIJIJINI KUTUMIA UMEME WA JUA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Watoto wa wafugaji wakiwa wanatizama Runinga ambapo taarifa ya habari ilikuwa hewani muda wa saa mbili za usiku baada ya kupelekewa umeme ...
Watoto wa wafugaji wakiwa wanatizama Runinga ambapo taarifa ya habari ilikuwa hewani muda wa saa mbili za usiku baada ya kupelekewa umeme wa jua na kampuni ya Mobisol ambapo fursa hii itawawezesha watoto waliopo vijijini kutambua fursa za maendeleo nchini
NA: ANDREA NGOBOLE, PMT

Kampuni ya Kimataifa ya umeme wa jua ya Mobisol ya Ujerumani, imetoa fursa kwa vijana wa vijijini ambao maeneo yao hayana umeme,kujiajiri katika kazi za kunyoa, kutokana na kuanza kusambaza mashine zinazotumia umeme wa jua huku ikitangaza kampeni ya kuhamasika na masika.

Akizungumza katika ofisi ya mwananchi jana, Meneja masoko wa kampuni ya Mobisol,Demetrius Wiston alisema, vijana wakitumia fursa zinazotokana na kampuni hiyo,wataweza kukabiliana na umasikini kwa kujiajiri wenyewe.

Alisema sambamba na huduma hiyo ya kunyoa, pia kampuni hiyo imeanza kusambaza luninga zinazotumia jua ambazo zinaweza kutumika kibiashara, mitambo ya kuchaji simu, radio na majokofu.

“huduma hii inapatikana katika mikoa 20 ambayo tunafanya kazi na lengo letu kuwa ni kufika vijiji vyote, maeneo ambayo jamii zipo nyuma”alisema

     Kampeni ya hamasika na masika.



Katika hatua nyingine, Kampuni hiyo,imeanzisha kampeni ya hamasika na masika, ambayo ina lengo la kuendesha bahati nasibu kwa wateja wake watakaonunua bidhaa mwezi April na Mei katika   mikoa 20 na zawadi zenye thamani ya milioni 4 zitatolewa.

Meneja  chapa  na uwezeshaji wa Mobisol Seth Mathemu alisema zawadi mbali mbali ikiwepo fedha taslimu,pikipiki na nyingine zenye thamani ya zaidi ya Sh 4 milioni zitatolewa.

Alisema mikoa ambayo itakuwa katika promosheni hiyo ni Arusha, Kilimanjaro na Manyara,Singida, Dodoma, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara, Kagera, Simiyu, Geita, Kigoma, Rukwa, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe,  Pwanipamojana Morogoro.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top