Na.Mwandishi
Wetu
Balozi wa Uingereza nchini
Tanzania, Sarah Cooke amesema nchi yake ipo tayari kuisaidia Tanzania katika
kutoa mafunzo maalum ya Menejimenti ya Maafa kwa wataalamu wetu.
Ameyasema hayo hivi
karibuni wakati alipomtembelea Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista
Mhagama ofisini kwake mjini Dodoma.
Akielezea lengo la ziara hiyo, Balozi Cooke alisema Serikali
yake inataka kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha inajipanga kukabili
na kurejesha hali pindi yanapotokea
maafa.
“Masuala ya maafa
yapo nchi nyingi ikiwemo kwetu Uingereza ingawa mafuriko na ajali za moto
zimekuwa zikiikumbaa nchi yetu mara kadhaa.”Alisema Balozi.
Aliongeza kuwa, Serikali ya Uingereza imevutiwa na juhudi zinazofanywa na Serikali
ya Tanzania katika kukabili na kurejesha hali ikiwa pamoja na kuwasaidia wananchi na mali zao pindi
yanapotokea maafa.
Kwa upande wake, Waziri Mhagama alimpongeza Balozi huyo
kuona umuhimu wa kuja Tanzania na kuonesha nia ya kuisaidia nchi kwa namna
mbalimbali.
Post a Comment