PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WAFUGAJI WALALA BARABARANI KUZUIA MSAFARA WA KAMATI YA BUNGE LOLIONDO.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mifugo ya wafugaji aina ya Ng'ombe wakiwa eneo la pori tengefu la loliondo kama walivyokutwa na kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Mal...
Mifugo ya wafugaji aina ya Ng'ombe wakiwa eneo la pori tengefu la loliondo kama walivyokutwa na kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira. uwepo wa mifugo hiyo katika pori hilo tengefu  umepelekea uharibifu mkubwa sana uhifadhi


wafugaji wa loliondo wakiwa wamejitokeza kuzuia msafara wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira mpaka watakapohakikishiwa kutoondolewa katika pori hilo tengefu kwa ajili ya malisho ya mifugo yao

 wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingiraa wakiwa wanapata maelezo juu ya mchanaga unaohama yaani shifting sand toka kwa mtaalamu Walter Mairo hayupo pichani




Baadhi ya wananchi wa Kata ya Arash wilayani Ngorongoro,  wamezuia msafara wa kamati ya bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii,kwa kulala barabarani wakipinga kutengwa eneo la pori tengefu kilomita za mraba 1500 ili lihifadhiwe.

Akizungumza mbele ya kamati hiyo, akiwa na wananchi wenye mabango,Mwenyekiti wa kijiji Mbuken, Parmitoro Mbotoony  alisema wanapinga mpango wa kumegwa ardhi hiyo kwani ndio tegemeo  la maisha yao ya kila siku.

Hata hivyo, wajumbe wa kamati hiyo,Richard Ndasa bunge wa jimbo la Sumve na mbunge wa jimbo la Siha,Dk Godfrey Mollel na mbunge jimbo la Babati mjini, Paulina Gekul waliwasihi wananchi hao, kuwa watulivu kwani maoni yao yamechukuliwa.

Akizungumza na wananchi hao,Dk Mollel aliwataka kuwa watulivu kwani,kamati hiyo haikufika Loliondo kuchukuwa ardhi ya vijiji na itahakikisha maslahi ya wananchi wa Loliondo yanalindwa .

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya tukio hilo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi  Atashasta Nditiye alieleza kusikitishwa na kitendo cha viongozi wa wafugaji kwahadaa wananchi na kuwaandaa ili kuifanyia vurugu  kamati yake.

Nditiye alisema nia ya ziara yao ya loliondo, haikuwa kufanya mikutano ya hadhara bali ni kulipitia eneo lenye mgogoro ili kujifunza na baadaye kutoa ushauri kwa serikali kwa maslahi mapana ya Taifa.

Hata hivyo, alisema walikutana na wawakilishi wa wananchi, wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro,Rashid Taka na kupokea maoni yao.

“tumewajua waliwapeleka wananchi kufunga barabara na kutaka kutufanyia vurugu na hasa baada ya kuwapotosha wananchi, sisi hatujaja kwa nia mbaya”alisema

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, akizungumzia mgogoro huo, alikanusha taarifa kuwa wizara yake imeiteka kamati na kueleza kamati ipo huru inatimiza wajibu wake.

“hii kamati imekuja  kuangalia maeneo ya hifadhi hasa kutokana na umuhimu wake kwani eneo hilo la ikolojia ya Serengeti linaingizia serikali dola milioni 200 kila mwaka”alisema

Mbunge wa jimbo la Mpanda mjini, Sebastian Kapufi, aliomba kamati hiyo ya bunge kuachwa huru ili itemize kazi yake ya kuishauri serikali kwa maslahi ya taifa.

Kwa zaidi ya miaka 20 kumekuwepo mgogoro wa ardhi,katika eneo la pori tengefu la Loliondo na safari hii mgogoro umelipuka kutokana na uamuzi wa wizara ya maliasili kutaka kutenga eneo la kilomita za mraba 1500 ndani ya eneo la kilomita 4000 za pori tengefu ili lihifadhiwe.

Eneo hilo linaelezwa kuwa ndilo lina vyanzo vya maji na ni mazalia ya wanyamapori katika eneo la ikolojia ya Serengeti.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top