Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauniakizungumza na
Maafisa na Askari wa vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyo chini ya
Wizara yake, katika Ukumbi wa Bwalo la Magereza, mjini Kilwa mkoani
Lindi. Masauni aliwataka maafisa na askari hao kuongeza nguvu zaidi
katika ukamataji wa wahamiajiharamu pamoja na wauza dawa za kulevya.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati),
akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga (kushoto)
wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa anakagua Makazi ya askari Polisi,
Mitwero mkoani humo ambapo nyumba za askari hao zimechangaa na chache
kutokana na wingi wa askari hao. Hata hivyo, Serikali hivi karibuni
inatarajia kujenga nyumba mpya katika eneo hilo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga akimuonyesha Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni eneola Mitwero mkoani
humo ambalo nyumba za makazi ya askari polisi zitakapojengwa. Masauni
alikagua nyumba wanazoishi askari hao kwasasa pamoja na kukagua eneo
hilo makazi mapya yatakapojengwa.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati),
akilikagua Jengo jipya la ghorofa la Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Lindi
ambalo linajengwa mjini humo. Kulia ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, George
Kombe, pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga.
Masauni aliongozana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyo
chini ya Wizara yake mkoani humo kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali
ya maendeleo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia),
akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga (wapili
kushoto), wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa anaangalia ramani ya
ujenzi wa makazi ya askari polisi eneo la Mitwero mkoani humo. Masauni
yupo mkoani humo kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (kulia) akimkaribishaNaibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ofisini kwake kwa ajili
ya kupewa taarifa ya mkoa huo, wakati Naibu Waziri Masauni alipofanya
ziara ya kikazi mkoani humo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Post a Comment