Raisi wa marekani katika hotuba yake aliyoitoa kuamkia leo kwa saa zetu
akihutubia baraza la Congress kuna mambo nimeona yanawagusa watanzania
mambo makubwa ni yafuatayo
1.Amesema BUY AMERICAN,HIRE AMERICAN akimaanisha kuwa ajira ni kwa
wamarekani na bidhaa watu wanunue za kimarekani au za makampuni ya
wamarekani wawe ndani ya marekani au nje ya wamarekani.Hii ina maana
kuwa kutakuwa na nafasi finyu mno kwa watanzania kuajiriwa marekani
katika utawala wa TRump kwani msisitizo wake utakuwa ni kuajiri
wamarekani na nafasi ya kampuni zisizokuwa za kimarekani kuuza bidhaa
zao marekani zitakuwa nafasi hizo finyu sana.
2.Kuhusu Biashara ya marekani na nchi zingine.Kasema Kampuni za marekani
zikiuza bidhaa nje ya nchi huwa wanachajiwa kodi kubwa sana kwa bidhaa
zao sehemu zingine hadi asilimia 100 hutozwa kodi kwa bidhaa zao wakati
bidhaa zinazotoka nchi hizo kuingia marekani hutozwa kodi kidogo au
hazitozwi kabisa.Amesema hilo hataliruhusu tena atahakikisha na wao
wakiingiza bidhaa zao marekani anawakomesha kwenye kodi.Hii ina maana
gani ni kuwa kama kuingiza gari la kimarekani Tanzania huwa tunatoza
ushuru wa asilimia mia moja tujiandae bidhaa zetu kuraruliwa kodi kwa
kiwango hicho hicho zikiingia marekani na kutazifanya bidhaa zetu
zisiweze kupenya na kushindana sokoni marekani
3.Amesema atatahakikisha inakuwa rahisi kampuni za marekani kufanya
biashara ndani ya marekani na atahakikisha inakuwa vigumu kwa kampuni za
marekani kutoka nje ya marekani kuhamisha mitaji na shughuli zao .Maana
yake ni kuwa ata encorage uwekezaji wa ndani na ku-discourage uwekezaji
nje ya marekani kwa kampuni za kimarekani.Hili lina maana kuwa kutakuwa
na upungufu wa wawekezaji wa kimarekani watakaokuja kuwekeza Tanzania
4.Kuhusu UHamiaji amesema anataka wahamiaji wenye uwezo wao wa kipesa
wenye pesa zao sio wale wanaotarajiwa kupata pesa za wamarekani.Anataka
wenye uwezo tu wa kifedha ndio wapewe kipaumbele .Maana yake ni kuwa
watanzania waenda kusaka fursa kule hawana nafasi tena Marekani anataka
kutumia utaratibu wa MERIT BASED kama unaotumika canada,austarlia na
newzeland
Post a Comment