Nikiwa mbele ya lango kuu la kuingia ndani ya hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro |
Baraza la wafugaji ngorongoro wakiwa katika ukumbi wa mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro |
Simba wakiwa wamejipumzisha n dani ya ngorongoro crater |
Simba wakiwa wamajipumzisha ndani ya Ngorongoro crater |
Kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira juzi imetua wilaya ya Ngorongoro na kulitembelea eneo la pori tengefu,ambalo linamgogoro kwa zaidi ya miaka 20 sasa ili kusaka suluhu.
Eneo hilo, lenye kilomita za mraba 4000,limeingia katika
mgogoro baada ya wizara ya Maliasili na Utalii, kutangaza uamuzi ya kutaka
kulitenga eneo la kilomita 1500 kwa ajili ya uhifadhi na eneo lililobaki
kurejeshwa kwa halmashauri ya Ngorongoro.
Akizungumza na waandishi wa habari, katika ziara hiyo,
Mwenyekiti wa kamati hiyo,Mhandisi Atashasta Nditiye alisema wamefika Loliondo
kuliona eneo hilo na baadaye watatoa ushauri kwa serikali.
Nditiye alisema wajumbe wa kamati hiyo, wamefanikiwa kupita
sehemu kubwa ya eneo hilo, ambalo linapendekezwa kugawanywa ili kutengwa eneo
la kilomita 1500 kwa ajili ya uhifadhi wa ikolojia ya Serengeti.
Akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati hiyo, Mhifadhi mkuu wa
hifadhi ya Serengeti, William Mwakilema alisema kwa manufaa ya Taifa na dunia
ni muhimu kutengwa eneo la kilomita 1500 ili lihifadhiwe.
Alisema eneo hilo ambalo ni mapito ya nyumbu
kutoka hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya, hadi Serengeti na baadaye
hifadhi ya Ngorongoro pia ndio eneo la
mazalia ya nyumbu na vyanzo vya maji,limeharibiwa sana mifugo na shughuli za
kibinaadamu na lisilipohifadhiwa uhai wa Serengeti upo mashakani.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa halmashauri ya Loliondo, Methew
Siloma alisema msimamo wao bado wanapinga kutengwa eneo hilo kwa kuwa ni la
vijiji na wanataka kutafutwa suluhu.
Mbunge wa jimbo la Geita ,Joseph Kacheku maarufu kama Msukuma
alieleza udhaifu uliopo katika kutunzwa eneo hilo lakini akataka ushirikishwaji
wa jamii ili kutambua umuhimu wa eneo hilo.
Wabunge wengine Grace Kiwelu na Lucy Owenya(viti maalum mkoa
Kilimanjaro) walitaka kutazamwa maslahi mapana ya taifa katika kulinda ikolojia
ya Serengeti.
Kwa
upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne
Maghembe, alisema dhamira ya serikali ni kuhakikisha Ikolojia ya Serengeti
inalindwa kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.
Post a Comment