PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MSD YAPATA FORKLIFT SITA KUTOKA GLOBAL FUND
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Forklift ikiwa kazini Na Dotto Mwaibale BOHARI ya Dawa (MSD) imekabidhiwa mashine za kupandishia mizigo juu na kushusha (Forklif...

Forklift ikiwa kazini

Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imekabidhiwa mashine za kupandishia mizigo juu na kushusha (Forklifts) sita, zenye gharama ya shilingi za kitanzania milion 531. 8, ambazo zimetolewa msaada na Mfuko wa Kimataifa wa Global Fund kupitia Shirika la Marekanila Ushirikiano wa Kimataifa (USAID).


Msaada huo ni sehemu ya awamu ya pili ya maboresho ya maeneo  ya kuhifadhia dawa ya MSD yaliyokuwa ya kifanywa na Global Fund, ikiwa ni  pamoja na upanuzi wa maghala ya kisasa yaani WiB ya MSD Makao makuu, Dodoma na Mbeya, na ujenzi wa maghala ya Kisasa MSD Kanda ya Tabora na Kituo cha mauzoTanga.

Wakizungumza katika makabidhiano hayo, yaliyofanyikaa jana katika utekelezaji wa awamu ya mwisho ya upanuzi na ujenzi wa maghala ya kisasa yanayojulikana kama Warehouse in -a –box, mashine hizo (forklifts), Naibu Mkurugenzi Mkazi wa JSI/SCMS Marasi Mwencha amesema fedha hizo ni zile zilizosalia kutoka kwenye ujenzi wa maghala ya kisasaya MSD, ambapo 
walikubaliana na menejimentiya MSD kununulia forklift.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amewashukuru wahisani hao kwa mashine hizo ambazo ni za gharama, na kueleza kuwa mashine hizo zitapelekwa kwenye kanda za MSD zenye uhitaji. 

Hata hivyo ameeleza kuwa tayari MSD ina Kiwanja  maeneo ya Luguruni, wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya kujenga ofisi na ghala la kisasa kwa Kanda ya Dar es Salaam hivyo wanategemea kuendelea kushirikiana na wahisani kwa ajili ya ujenzi pindi taratibu zitakapokamilika.

 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top