Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe John Mongella akizindua rasmi tawi la Nyanza-Mwanza na lile la Uluguru-Morogoro
Naibu
Mkurugenzi mtendaji wa Bank of Africa Tanzania Wasia Mushi akimkabidhi
mkuu wa mkoa wa Mwanza zawadi ya Visa Prepaid Card (TOUCAN CARD) ambayo
itamwezesha mkuu huyo wa mkoa kufanya online purchases pamoja na kupata
huduma za kifedha kwenye ATM machine Zaidi ya Milioni tatu zilizopo
sehemu mbalimbali duniani.
Naibu
Mkurugenzi mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Wasia Mushi akitoa
hotuba katika uzinduzi wa matawi mawili ya Bank of Africa Tanzania
Mwanza na Morogoro. Uzinduzi wa matawi haya unafanya benki hiyo kua na
jumla ya matawi 27 nchi nzima.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella akitoa hotuba yake katika halfla
ya uzinduzi rasmi wa matawi mawil ya Bank of Africa Tanzania.
Akizungumza
mkoani Mwanza, wakati akizindua matawi mawili kwa pamoja ya Bank of
Africa Tanzania tawi la Nyanza lililopo jijini Mwanza na wakati huo huo
tawi la Uluguru lililopo jijini Morogoro, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh.
John Mongella alisema ni wakati wa wanaMwanza kutumia huduma za kibenki
na kwamba Mwanza ni ya pili kuchangia katika pato la taifa.
“Nimesikia
kwamba mna matawi 27, huu ni wakati wa wanaMwanza kutumia huduma za
kibenki. Naomba mfahamu kwamba Mwanza inachangia asilimia 7 ya pato la
taifa. Bank of Africa Tanzania natambua kuwa mnasaidia juhudi za
serikali kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi,”alisema Mh. Mongella.
Awali
akizungumza kabla ya ufunguzi wa matawi hayo kwa pamoja, Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Wasia Mushi alisema :
“Benki ya Afrika ipo katika nchi 18 na kwamba makao yake makuu yapo
Dakar, Senegal. Hapa nchini ina makao yake makuu jijini Dar es Salaam na
jumla ya matawi 27.”
Mushi
alisema katika kipindi cha miaka 10 benki hiyo imekuwa benki muhimu,
imara endelevu kwa kutoa huduma zake za kibenki kwa watu mbalimbali
wakiwamo wateja wakubwa, wadogo na wa kati.
“Mwanza
inajulikana zaidi kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uvuvi
katika Ziwa Victoria, uchimbaji wa madini, kilimo cha pamba na utoaji wa
huduma katika sekta mbalibali, hivyo ni muhimu wakatumia huduma za Bank
of Africa Tanzania,”alisema.
Alisema
benki hiyo imedhamiria kuleta mapinduzi kwenye sekta za kibenki kwa
kutoa huduma stahiki ambazo zitaweza kumfikia kila Mtanzania kwa njia
nyepesi kupitia wafanyakazi wao.
“Tawi
la Nyanza na tawi la Uluguru yote yamefunguliwa kwa pamoja, hii ni
benki ya biashara ambayo imeanzishwa mwaka 2007. Leo ina matawi 27
katika maeneo mbalimbali nchini”
Alisema
kwa sasa benki hiyo inatoa mikopo mbalimbali ikiwamo ya ukarabati wa
nyumba, kutumia nyumba kama dhamana ya kupata mitaji ya biashara au
kusaidia kujenga nyumba nyingine.
“Kwa
pamoja Bank of Africa Tanzania imeungana na shirika la maendeleo la
Ufaransa AFD kwa manufaa ya kuwezesha watu mbalimbali wanao jikita
kwenye shughuli za nishati endelevu na mbadala,”alisema Mushi.
Post a Comment