Goli la mshambuliaji Deus Kaseke
limeivunja Yanga kuvunja mwiko wa miaka 30 zaidi katika uwanja wa
Majimaji mkoani Ruvuma na kuondoka na alama tatu muhimu mchezo wa Ligi
kuu Vodacom Tanzania bara dhidi ya wenyeji Majimaji.
Dakika ya 14 Kaseke alifunga goli
baada ya mlinda mlango wa Majimaji kuutema Mpira uliokuwa umepigwa na
Nahodha wa Yanga Haruna Niyonzima na kumkuta mfungaji akiwa katika hali
nzuri na kuweza kutikisa nyavu za wenyeji.
Simon Msuva na Amis Tambwe
wangeweza kufunga magoli mengi zaidi kutokana na kukosa nafasi nyingi za
wazi hadi Mapumziko Yanga walienda wakiwa kifua mbele kwa goli hilo
moja.
Kipindi cha pili kilikuwa kigumu
kwa kila timu na kupelekea kufanya mabadiliko mbalimbali huku Yanga
wakicheza kwa kushambulia na kukaba zaidi kutokana na Mpira kukosa radha
kutokana na ubovu wa uwanja huo.
Mpaka dakika 90 Mwamuzi Hussein
Athumani anapuliza kipyenga cha mwisho Yanga wameibuka na pointi tatu
muhimu na kuweza kumsongelea mtani wake Simba ambaye anaongoza Ligi Kuu.
Kwa Matokeo hayo Yameifanya
Majimaji kuwa katika Mstari wa kushuka daraja hivyo wanatakiwa
kubadilika kwa mechi ambazo zimebaki wakati Yanga wamefikisha pointi 43
nyuma ya moja dhidi ya Simba wenye 44.
Ligi Kuu ya Tanzania inatarajia
kuendelea tena kesho kwa michezo miwili kucheza katika viwanja
mbalimbali macho ya wengi yatakuwa mkoani Morogoro Mtibwa Sugar
watawakaribisha Vinara wa Ligi timu ya Simba wakati Mabingwa wa Kombe la
Mapinduzi Azam FC watacheza na Mbeya City majira ya saa moja usiku
kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es
salaam.
Kikosi cha Yanga
; Deogratius Munish ‘Dida’, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Andrew Vincent,
Kelvin Yondani, Thaban Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Oscar
Joshua dk90, Amissi Tambwe, Juma Mahadhi na Deus Kaseke/Said Juma
‘Makapu dk’80.
Maji Maji; Agathon Anthony, Salehe Mohammed, Mpoki Mwakinyuke, Keneddy Kipepe, Bahati Yussuf/Emmanuel Semwanza dk25, Yakoub Kibiga/Paul Nyangwe dk58, Iddi kipwagile, Kelvin Kongwa, George Mpole, Hassan Hamisi na Lucas Kikoti/Peter Mapunda dk46.
Post a Comment