PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MTU YOYOTE YULE ANAWEZA KUWA BINGWA KATIKA JAMBO LOLOTE ALITAKALO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA: ANDREA NGOBOLE PMT Heri ya mwaka mpyaaa wa 2017 ndugu msomaji wa princemediatz blog, facebookpage na instargram ni matumaini ...


https://scontent.fjnb2-1.fna.fbcdn.net/v/t1.0-9/426858_255089914582518_871807701_n.jpg?_nc_eui2=v1%3AAeGSfpkRJii1b2LLm7vhRsU6iYxttkBoCIOxg3yUgAUzGaW4kUkMNOjpnXk-WCzHna1hs8kp6JpjBb3X5yuJpc_YvrWgJf1CSOew8kuPc5Yw78BGFrNUrebvTxy56zObj4A&oh=d35f811134c2cf8601888d9ab06ffb6a&oe=59188166

NA: ANDREA NGOBOLE PMT
Heri ya mwaka mpyaaa wa 2017 ndugu msomaji wa princemediatz blog, facebookpage na instargram ni matumaini yangu kuwa umeuanza mwaka vyema na hatuna budi kumshukuru Mungu kutujalia afya na uzima tele.

Leo nimeona tushirikishane jambo moja kubwa nalo  NI ukweli usiopingika ya kuwa kila mmoja wetu hupenda kuwa mtaalamu wa jambo Fulani ila sasa njia za kuwa bingwa katika jambo husika ndio tabu kuu inayowakabili wengi kwani hatufahamu ni kwa namna gani tunaweza kuwa wataalamu wabobezi katika fani husika.

Mathalani unapenda kuwa mtaalamu wa uchumi, siasa, uandishi wa habari na kadhalika huna budi kwenda chuoni kujifunza utaalamu husika ambapo ni jambo zuri kwani utakuwa ,mtaalamu wa taaluma husika lakini huwezi kuwa bingwa wa taaluma hiyo; sasa huenda hujanielewa naposema kuwa bingwa katika taaluma husika ninamaanisha kuwa uwe mtaalamu mbobezi katika fani husika ndio maana ukienda hospitali kuna madaktari na madaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama na watoto, wa mifupa, saratani na kadhalika hii hutokea baada ya wao kujipambanua katika jambo Fulani na kutilia mkazo katika fani husika sasa na wewe unaweza kuwa bingwa katika jambo lolote unalotaka kuwa kama utafanya yafuatayo
Image result for mayagila joseph
Joseph Mayagila mkurugenzi wa mafunzo chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha( AJTC) akifundisha katika moja ya semina zilizofundishwa chuoni hapo mwaka 2015 na wanaoonekana pichani pia ni baadhi ya wakufunzi wa chuo hicho wakimsikiliza kwa makini
 Image result for mayagila joseph
Kwa mujibu wa Joseph Mayagila Mkurugenzi wa mafunzo chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) anasema Ili uwe bingwa katika jambo unalolitaka unatakiwa uwe na kitu kinachoitwa ONE HOUR HABIT yaani hii ni tabia utakayoijenga ya kuwa na saa moja la kuifunza jambo hilohilo kila siku katika maisha yako yote na huo muda lazima uuheshimu. 

Kwa mfano kwa siku  moja kuna saa 24 lazima utenge saa 8 za kufanya kazi kama umeajiriwa saa 8 za kufanya shughuli zako binafsi mbalimbali kama utakavyojipangia na saa 8 za kupumzika kwa maaana ya kulala ili kuupumzisha mwili wako na ubongo wako uweze kufikiria mambo ya maendeleo yajayo. 

Sasa katika yale masaa 8 ya kufanya shughuli zako binafsi tenga saa moja kwa maana ya dakika 60 za kujifunza jambo moja ambalo unatamani kuwa bingwa kwa mfano ukitaka kuwa mwanasheria bingwa wa sheria za ardhi inabidi usome vitabu mbalimbali vinavyohusiana na sheria hizo pia ukitaka kuwa mjasiriamali pia jenga utamaduni wa kusoma vitabu vinavyozungumzia maswala ya ujasiriamali vilivyoandikwa na watu waliofanikiwa katika maswala ya  biashara mfano vitabu vya Donald TRUMP ambaye kwa sasa ndiye Raisi mteule wa Marekani 

Mwanzo utakuwa mgumu sana ila jitahidi kwa siku 21 mfululizo ujipe saa moja kujifunza hicho kitu unachotamani kuwa bingwa na muda mzuri Zaidi  ni saa tatu mpaka saa tano za usiku chagua muda sahihi kwako kabla ya kwenda kulala uwe tayari umejifunza kitu katika jambo husika na ukiweza kujenga mazoea ya kusoma vitabu hivyo kila siku kwa hizo siku 21 basi utajenga tabia na ikishakuwa kuwa tabia utajenga mazoea kasha kuwa utamaduni ambao utakufanya ufahamau mambo kwa upana Zaidi juu ya fani husika na ukiweza kufanya kwa miezi 12 mfululizo mwisho wa siku utakuwa bingwa wa taaluma husika ndio utakuwa bingwa wa jambo hilo ulitakalo mmhhh sasa unaweza kuwa mvivu wa kusoma vitabu ila siku hizi mambo yamerahisishwa mno kwani kupitia mitandao ya kijamii kuna Makala mbalimbali zinazozungumzia mada inayohusiana na jambo ulitakalo kujifunza pia vipo vitabu vilivyorekodiwa kwa sauti unaweza kusikiliza na mwisho wa siku kuna jambo utakuwa umejifunza na ukilifanyia kazi utakuwa mtaalamu mbobezi katika jambo husika.

Kwa mfano mie ni mwalimu ili niendele kuwa mwalimu bora Zaidi sina budi kujifunza jinsi walimu wanavyofundisha darasani pia kwenye semina za ujasiriamali, mafunzo ya mikutano ya injiili mfano mwalimu Mwakasege anavyofundisha katika mikutano yake kwa hiyo kila siku ninasoma vitabu vinavyoelekeza jinsi ya kufundisha na pia jinsi kuwaelewa wanafunzi wangu kama wamenielewa katika somo ninalofundisha, ninajifunza kila siku juu ya somo ninalofundisha  kwa kuongeza maarifa mapya yatakayonisaidia kuweza kueleweka mbele ya wanfaunzi wangu nikiwa kanisani najifunza nikiwa mtaani pia najifunza ili kuunoa Zaidi ubongo wangu.

Hivyo basi unaweza kuwa mtaalamu mbobezi ama  bingwa katika jambo lolote lile ulitakalo kama tu utajipa muda wa saa moja la kujifunza kitu kimoja kila siku mpaka uwe muelewa bingwa wa jambo husika, jiulize mtu kuandika kitabu mpaka kikamilike humchukua si chini ya miezi mitatu na ameshirikisha akili za watu wengi mpaka kukamilika kwa kitabu hicho wewe unapokisoma kwa siku moja au saa moja unakuwa umefyonza ubongo wake na maarifa yake ya miezi kadhaa kwa siku moja hapo unakuwa umeongeza maarifa makubwa sana na utaweza kuwa  bingwa wa taaluma husika kama utasoma vitabu na mada Zaidi ya ishirini kwa mwezi mmoja na hii haihitaji kulipia ada kwani ni elimu kubwa unayoipata bure kabisa kwa kujipa muda wa kutosha kjifunza jambo jipya kila siku.

Mwaka huu wa 2017 uwe na lengo moja kubwa nalo ni kuwa bingwa katika jambo ulitakalo anza taratibu na utajikuta unakuwa bingwa wa jambo hilo kama ni mwanamuziki uwe na saa moja ya kujifunza kuimba, kama ni mwandishi kila siku uwe unaaandika Makala moja, kama ni mkulima kila siku uwe na saa moja ya kupata maarifa ya ukulima bora wa zao husika vivyo hivyo katika tasnia yoyote uitakayo naamini utakuwa bingwa wa mabingwa.

Asante kwa kusoma makala hii uwe na mwaka wenye mafanikio tele
NGOBOLE, Andrea Ashery.
0755780131

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top