USIKU wa Jumanne ya Aprili 15, 2012
vijana wawili wachezaji wa soka wanabishana kuhusu kuondoka mahali
walipokuwa ili wakapumzishe miili yao baada ya pirika za kutwa nzima.
Hao ni viungo wa soka, Ramadhan Chombo ‘Redondo’ na Patrick Tabu Mutesa
aliyekuwa maarufu kama Patrick Mutesa Mafisango ambaye kwa sasa ni
marehemu.
Kwa mujibu wa Redondo, Mafi sango alitaka
waendelee kukaa katika klabu moja ya usiku kwa muda kidogo lakini kwa
kuwa ilishakuwa usiku sana yapata saa 7:00, yeye alimsihi waondoke na
kweli wakaondoka. Haikuwa rahisi kwa Mafisango kuondoka mahali hapo
lakini ushawishi mkubwa wa Redondo uliwezesha wawili hao kuondoka na
kurudi nyumbani kupumzika.Wachezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mafisango.
KIONGOZI SIMBA ATOA FEDHA
Asubuhi ya Jumatano Apri- l i 16, 2012
akiwa ny- umbani kwake Chang’ombe jijini Dar es Salaam, Mafi sango
aliletewa fedha na kiongozi mmoja wa Simba kwa ajili ya matumizi
mbalimbali. Baada ya kupokea fedha hizo, Mafisango akiwa na Redondo
alianza kulazimisha waanze kupata ‘moja moto moja baridi’ lakini
mwenzake alikataa hadi watakapopata chakula cha mchana.
“Alionekana kutaka kinywaji sana lakini
nilimsihi kwamba si vizuri kutumia kinywaji muda huo badala yake asubiri
hadi tutakapopata chakula cha mchana kwanza,” anasema Chombo. Baadaye
Mafi sango aliletewa gari Toyota Chaser GX 100 kwa ajili ya kulitumia
siku hiyo, lakini mpwa wake Orly Ilemba na Ally Hassan ‘Bozy’ walitoka
na gari hilo kwenda Magomeni. Baada ya kuwasubiri kwa muda mrefu, Mafi
sango na Redondo waliamua kuwafuata Magomeni akina Orly baada ya kuona
wanachelewa kurejea Chang’ombe na gari hilo.Lari lakebaada ya ajali.
MAFISANGO APIGA USINGIZI WA AJABU
Walipofi ka Magomeni, Mafi sango na
Redondo waliungana na akina Orly kisha wakalekea Kinondoni ambako
walipata chakula lakini jambo la kushangaza baada ya kula, Mafi sango
alilala usingizi mzito. “Wakati analala nikawaambia watu tuliokuwa nao
kwamba wamuache apumzike na alilala usingizi mzito sana hadi
alipozinduka baada ya kama saa mbili hivi,” anasema.
Kabla ya kula Mafi sango aliwarushia
maneno akina Orly ambao hawakuonyesha hamu ya kula chakula hasa baada ya
kuwasema kwa kuchelewa kuwafuata Chang’ombe.AGAWA FEDHA NA KUAGA
Karibu muda mwingi wa mchana, Mafi sango
alikuwa akitoa fedha au vinywaji kwa watu huku akisema kwa utani,
kunyweni hamjui labda ndiyo tunaagana au maisha haya mafupi sana. Hata
fedha alikuwa akitoa kwa baadhi ya watu aliokuwa akifahamiana nao na
karibu wote alikuwa akiwapa na kuwaambia maneno hayo.
“Sisi tuliona kama
kitu cha kawaida lakini kumbe yeye sijui kuna kitu alihisi au la,
lakini alikuwa akitoa fedha na kutamka maneno ya kuaga,” anasema Bozy.SAFARI YA MAISHA CLUB
Mafisango alikuwa na asili ya DR Congo
licha ya kuwa na uraia wa Rwanda, alihamia Rwanda akiwa mkubwa na ni
katika harakati za maisha ya soka tu. Huko ndiko alikopata jina la Mafi
sango ambalo ni la ukoo wa mwanamke aliyezaa naye mtoto mmoja aitwaye
Crespo, hivyo Mafi sango alitumia jina la mkwewe.
“Safari ya kwenda Maisha Club ilianzia
katika Pub moja iliyopo Kinondoni ambapo tulikuwa watu kama sita au saba
kwani walikuwepo Bozy, Orly, Nyomaa (Gaspar Karemera) na wanawake
wawili akiwemo Zai ambaye alikuwa akituhudumia vinywaji. “Lakini Zai
alijiunga nasi katika ile hali ya kawaida ya kampani na ilikuwa mara
yetu ya kwanza kwenda naye club,” anasema Redondo.
ATUNZA FEDHA NA CHENI YA THAMANI
Wakiwa Maisha Club katika onyesho la
Bendi ya Muziki wa Dansi ya FM Academia, Mafisango alikuwa akitunza fedha
kila mara na waimbaji wakawa wanamuimba. Bozy ndiye aliyekuwa akitumwa
fedha hizo kuzipeleka kwa waimbaji na ilifi ka wakati kabla hata ya kuwafi
kia walikuwa wakianza kumuimba Mafisango.
Ndipo ulipofi ka muda alitoa cheni yake
ya silva ili nayo ipelekwe kwa muimbaji mmoja, lakini Bozy akahoji vipi
aitoe cheni hiyo? Lakini akaambiwa; “Peleka”. “Alinipa cheni yake ya
silva ili nikamtunze muimbaji mmoja, ilikuwa ya gharama na nilipomuuliza
akaniambia nimwambie muimbaji yule kwamba hiyo ni kumbukumbu yake kwani
wanaweza wasionane tena.
“Tangu
mchana alisema anataka kutumia fedha zote alizonazo siku hiyo hadi
ziishe ndipo arejee nyumbani, na kweli hilo alilitekeleza,” anasema
Bozy. Mafi sango alikuwa akigawa dola 100 (sasa ni zaidi ya Sh 220,000)
kwa watu mbalimbali aliokutana nao na hata klabu alikuwa akitoa fedha
hizo kwa waimbaji ambao walikuwa rafi ki zake.
REDONDO AONDOKA KLABU
Kabla ya saa 8:15 usiku, Redondo na rafi
ki wengine wa Mafi sango waliondoka Maisha Club kwa kutumia usafi ri
mwingine wa kukodi na kuwaacha wao watano yaani Mafi sango, Orly, Bozy,
Nyomaa na yule dada Zai. Waliendelea na burudani huku wakinywa na kabla
ya kuondoka, Orly na Bozy walikuwa hawaonekani ndipo Mafisango na yule
dada wakatoka nje wakitaka kuondoka.
Baadaye akina Orly waliporudi walipoketi
kina Mafi sango na kutowakuta, waliamua kwenda nje kuwafuata ndipo
walipomkuta kiungo huyo wa zamani wa Simba akiwa amekasirika na kutaka
funguo zake za gari huku akiwataka waondoke.
“Tangu asubuhi mimi ndiye niliyekuwa
naendesha gari kwani Mafisango hakuwa mzoefu wa kuendesha gari Dar es
Salaam hasa barabara kuu, nilisita kumpa funguo ili atuendeshe lakini
sikuwa na jinsi. “Aliniambia yeye ndiye mwenye gari hivyo nimpe funguo,
halafu kama kuna kitu kibaya anataka kimtokee yeye mwenyewe na siyo mtu
mwingine pia alisema anataka aendeshe gari hilo mpaka mwisho wake.
“Hatukuelewa ana maana gani ila tuliona
ni jambo la kawaida tu, nikampa funguo na safari ya kurejea nyumbani
ikaanza,” anasema Bozy. Kabla ya kuelekea Chang’ombe walipitia Kinondoni
kwanza kwa Redondo kumjulia hali kama amefi ka salama halafu wakaendelea
na safari yao.
PALE KEKO KUMBE WALIGONGWA
Tofauti na ilivyoripotiwa awali kwamba
Mafi sango alikuwa akiikwepa baiskeli ya matairi matatu maarufu kama
Guta, ukweli ni kwamba waligongwa na gari lingine kwa nyuma.
Kama ilivyoelezwa awali kwamba, Mafi
sango hakuwa na uzoefu sana barabarani hivyo baada ya kugongwa licha ya
kuzidiwa na gari, asingeweza kuchukua hatua yoyote ile zaidi ya kuacha
gari liende linavyotaka. “Ukweli kabla ya ajali ile kuna gari
lilitugonga nyuma na dereva wa gari letu ambaye ni Mafi sango alipoteza
uelekeo. “Baada ya kugongwa, Mafi sango alipoteza uelekeo na gari
likaenda kugonga mti lakini kilikuwa ni kishindo kikubwa mno, gari
lililotugonga halikuwa kubwa kama yale y a mizigo bali lilikuwa gari la
saizi ya kati kama Nissan Patrol lakini lenye ngao kwa mbele.
“Baada ya kile kishindo mimi nilipoteza
fahamu kwa muda kama wa dakika mbili hivi na nilipozinduka nikajikuta
nipo nje ya gari chini ya mchanga, nikarudi katika gari na kumkuta Mafi
sango ameumia akiwa ameinamia usukani,” anasema mmoja wa abiria
waliokuwemo ndani ya gari hilo. Bozy aliyekuwa kwenye gari hilo wakati
wa ajali, naye alithibitisha maneno ya abiria mwenzake kwa kusema: “Ni
kweli tuligongwa kwa nyuma na gari lililotugonga lilikimbia.
“Ninachokumbuka ni kwamba Mafisango
alikuwa akiendesha kwa mwendo wa spidi kati ya 80 hadi 100 na hakuwa
mzuri sana barabarani, lakini licha ya kutokuwa na uzoefu na barabara za
Dar es Salaam, huku mwanzo hakuweza kusababisha ajali hadi tulipofi ka
Keko na kugongwa. “Lakini inauma sana kwani sielewi Mafi sango alikufaje
kwani wote hatukuwa tumefunga mikanda ya usalama,” anasema Bozy.
Abiria wote yaani Zai, Nyomaa, Orly na
Bozy hawakuumia sana na wala hawakutibiwa kwa muda mrefu, lakini Mafi
sango alionekana kuumia sana kichwani katika paji na jichoni. Ikumbukwe
kuwa Bozy si aliyetoa maelezo Polisi bali ni Orly na Nyomaa ndio
waliofanya hivyo.
Hakika hizo ndizo saa 24 za mwisho za Mafisango!
Post a Comment