Jiji la Nairobi limetajwa kushika nafasi ya 9 ya majiji yenye foleni zinazoongeza kiwango kikubwa cha hewa chafu ya Carbon dioxide na zinazokera duniani.
Utafiti uliofanywa na mtandao wa Numbeo umezingatia kiwango cha muda unaotumiwa na magari ya kusafirisha abiria kila katikati ya miji na kuonesha kwamba wastani wa chini wa muda unaotumiwa na abiria kwenye foleni ni dakika 65.20 kwa kila safari moja.
Kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Kenya zilizotolewa mwka huu mwezi wa Tano zilionesha kuwa Serikali inapoteza kiasi cha shilingi milioni 58.4 za Kenya kwa siku ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni moja za Tanzania kutokana na foleni za magari nchini humo.
Kwa Africa, Nairobi imeshika nafasi ya tatu ikiwa nyuma ya jiji la Pretoria kutoka Afrika Kusini na jiji la Cairo nchini Misri
Hii ndio Top 10 ya majiji yenye foleni zaidi duniani.
1. Manila, Philippines – Dakika za kusubiri foleni: 54.33
2. Pretoria, South Africa – Dakika za kusubiri foleni: 52.25
3. Recife, Brazil – Dakika za kusubiri foleni: 57.85
4. Tehran, Iran – Dakika za kusubiri foleni: 59.84
5. Miami, Florida – Dakika za kusubiri foleni: 59.20
6. Kolkata, India – Dakika za kusubiri foleni: 58
7. Cairo, Egypt – Dakika za kusubiri foleni: 58.61
8. Pune, India – Dakika za kusubiri foleni: 60.86
9. Nairobi, Kenya – Dakika za kusubiri foleni: 65.20
10. Mumbai, India – Dakika za kusubiri foleni: 66.18
Post a Comment