NA: SIMON MJEMA, SAME
Rai imetolewa kwa Waendesha bodaboda Mkoani Kilimanjaro
kutii sheria bila shuruti kwa kujitambua na kujithamini,kwa lengo la kuokoa
vifo visivyo vya lazima,hali itakayopunguza vifo vya akina Mama Wajane na
Watoto Yatima wanaotokana na Bodaboda kutokutii sheria.
Rai hiyo imetolewa na Katibu wa Bodaboda Mkoa wa
Kilimanjaro,Rashidi Omary,wakati akihojiwa na Waandishi wa Habari,katika ukumbi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Same kwenye Mkutano wa Mkuu wa Wilaya hiyo,Rosemary
Staki Senyamule na waendesha bodaboda Same;Ambapo Katibu huyo ameliomba Jeshi
la Polisi kusimamia sheria kwa kuwachukulia hatua wale wote wanaovunja sheria
za usalama barabarani.
Mkuu wa Wilaya ya Same,Rosemary Staki Senyamule,amesema
bodaboda ni ajira hivyo inawapasa kutii sheria za Usalama barabarani kwa kuhakikisha wanavaa kofia ngumu,kutokubeba
mshikaki na taratibu zingine za sheria za barabarani.Ambapo pia amewataka
kutumia fursa za mikopo zinazopatikana Serikalini na kwenye Taasisi za Kifedha
kama Benki.
Petro Gichinja ni mwendesha bodaboda Mjini Same,ameliomba
Jeshi la Polisi kusimamia haki katika utekelezaji wa majukumu yake ili
kuepukana na Tabia ya baadhi ya Watumishi wa Serikali kuendesha pikipiki bila
kufuata sheria kama vile kutokuvaa Helmenti,huku boda boda wao wakikamatwa pindi
wanapovunja sheria hizo.
Post a Comment