Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Katika
maisha ya kila siku tunakutana na changamoto nyingi,misukosuko mingi ambayo wakati mwingine inatukatisha tama na
kutupunguzia spidi ya mafanikio.
Ni ukweli
usipingika kuwa tunahitaji muda wa ziada wa kujirepea mithili ya gari lililotembea umbali mrefu na kupita katika makorongo,milima,mabonde
na changarawe.
Baada ya
mapito yote hayo unahitaji kufanyiwa matengenezo na maboresho ili uwe imara
tena uweze kuhimili mitikisiko ya safari ya maisha.
Kujirepea ni
muhimu ili uweze kurudi kati hali yako nzuri itakayokuwezesha kufanya vizuri
katika maisha.
Bila
kujirepea ni vigumu kupata nguvu ya kutosha kukabiliana na magumu katika maisha
na kuyashinda lasivyo hali itakua ngumu
unaweza kufa moyo ama kuishia njiani katika safari yako ya mafanikio ya
kibiashara,kielimu,kifamilia na kiuchumi.
Mambo Magumu
tunayoyapitia duniani hayatuachi tulivyo yanaondoka na kitu cha thamani ndani
yako haijalishi ni kikubwa au kidogo hivyo unahitaji muda wa kurejesha thamani
iliyopotea ndani yako.
Ni muhimu
kutenga muda wa kujifariji mwenyewe,kufarijiwa na kufarijiana ,kutiana moyo ili
tuweze kusonga mbele katika safari ya maisha na kufanikiwa.
Ni vyema
kujisomea vitabu vitakavyojenga mtazamo chanya ndani yako ,matumaini
mapya,tazama video na kusikiliza sauti ambazo ni chanya zitakazokupa hamasa ya
kutimiza malengo yako.
Unahitaji
kukaa mazingira tulivu yenye ukimya ,mazingira yanayoponya (healing inviroment) unashauriwa iwe ni mbali
kidogo namazingira ya nyumbani ambayo
umeyazoea ,mazingira yenye kijani ,uoto wa asili,maji,chem chem kwa kutazama
maji pia unaweza kupunguza msongo wa mawazo.
Pata Muda wa
kujisikiliza ,kusikiliza sauti iliyoko ndani yako inayokukumbusha juu ya kusudi
la maisha yako duniani kwamba uko duniani kwa kazi maalumu hauko duniani kama
kwa bahati mbaya ama ajali ya kibailojia.
Chukua Muda
wako Kujitathmini juu ya maisha yako ya kila siku namna unayoongea na
watu,unavyowatendea watu,unavyojitendea wewe mwenyewe,kazi
,mahusiano,uchumi,biashara .
Je? Umefika unapotaka
kufika? ,njia unazopita zitakufikisha pale unapotaka kufika? Uongeze nini ?,upunguze
nini? Ubunifu wa aina gani unahitajika kuboresha huduma yako,kazi yako na
maisha yako kwa ujumla.
Pata muda wa
kuwasamehe waliokukosea na kujisamehe pia pale ulipojikosea ,Kwasababu ili kuishi
maisha yenye furaha sharti moja wapo la kuzingatia ni kusamehe kila kukicha.
Kusamehe ni
muhimu kwasababu katika mikiki mikiki ya maisha kuna mikwaruzano ,kukanyagana
ili mradi kuyafikia maisha yako.
Chukua muda
wako kuwashukuru wale wote ambao wamekua wema kwako kwa namna moja au nyingine
na kuchangia kukufikisha hapo ulipo ,shukuru hata kwa machache utakirimiwa
mengi.
Tumia muda
wako wa ziada kuboresha kazi yako,biashara yako,kipaji chako ili kuleta manufaa
tarajiwa.
Jifunze
mbinu mpya za mapambano nje ya uwanja wa mapambano ili ukiingia kwenye uwanja
wa mapambano uweze kushinda .
Ibua ubunifu
mpya na utofauti utakaokuwezesha kuliteka soko
acha kufanya mambo ya kawaida kila siku yanayofanya maisha yako kuwa ya
kawaida,biashara ya kawaida,uchumi wa kawaida,Kataa kuwa wa wakawaida,kuwa
Mbunifu kuwa wa Tofauti.
Tumia muda
wako wa ziada kujifua mithili ya mwanajeshi anayejua mbele yake kuna vita ya
maisha na anahitajika kupambana na kushinda .
Tumia muda wako wa
ziada kutengeneza ushindi wa kesho
hata kama leo ulishindwa.
Maisha ni
kama mchezo leo unaweza kushindwa kesho ukashinda usikate tamaa jiandae
kushinda.
Tumia muda
wako kwa nidhamu ,tumia fedha zako kwa nidhamu,tumia nguvu zako kwa
nidhamu,tumia akili zako kwa nidhamu.
Nakutakia
Ushindi na Mafanikio katika Kila jambo jema la kimaendeleo
0765938008
Post a Comment