Professor Jay akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) ya EATV amedai kuwa wasanii wengi wa kipindi hiki kazi zao za muziki zimekuwa zikizidiwa na kiki wanazofanya jambo ambalo linapelekea wasanii hao kushindwa kufanya vizuri kwenye sanaa, na kuachia nyimbo mara kwa mara kwa kuwa kazi hizo zinakuwa hazina nguvu, wala ubora kutokana na wasanii hao kutegemea kiki ili kufanya vizuri.
"Wasanii wengi wa sasa wanasumbuliwa na hizi kiki, unakuta msanii ana wimbo lakini kiki zake ni kubwa kuliko hata hizo nyimbo zake, yaani ni sawa na mtu anakimbia mpaka anapitiliza kwake. Hizi kiki za wasanii hawa ni jambo ambalo linapelekea wasanii hao kujikuta wanatakiwa kutoa kazi mpya kila siku maana kazi zao zinakuwa hazina nguvu kama kiki zao" alisema Professor Jay
Mbali na hilo Professor Jay alisema kuwa yeye mpaka sasa anazaidi ya 'Hits song' 100 lakini hata sikumoja hajawahi kutegemea kiki katika kufanya kazi zake zaidi ya kutengeneza ngoma kali.
Post a Comment