Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP), Mohamed Mpinga (wa pili kushoto), akizungumza na wamiliki wa shule za udereva (hawapo pichani), wakati akifungua mkutano wa pili wa Chama cha Shule Binafsi za Udereva Tanzania (Chashubuta), Hoteli ya Dreamers Buguruni Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (ASP), Deus Sokoni, Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Robert Mkolla na Katibu wa chama hicho, Jonas Mhati
Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Robert Mkolla (katikati), akimkabidhi risala yao Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP), Mohamed Mpinga. Kulia ni Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (ASP), Deus Sokoni.
Katibu wa chama hicho, Jonas Mhati (kushoto), akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa chama hicho, Jonas Mhati (kushoto), akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mjumbe wa chama hicho, Cosmas Munuo (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo.
Mjumbe wa chama hicho, Regina Sulle akiuliza swali kwenye mkutano huo. Kushoto ni mjumbe Fatma Somji na kulia ni Santos Akyo.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP), Mohamed Mpinga (kushoto), akisisita jambo wakati akijibu maswali ya wanachama wa chama hicho. Kulia ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Robert Mkolla.
Mjumbe wa mkutano huo, Leonard Mtandika akiuliza swali. Kutoka kulia ni Pascol Mtandika na Ibrahim Nyato.
Mjumbe wa Mkutano huo kutoka mkoani Dodoma, Robert Mwinje (kulia), akichangia jambo kwenye mkutano huo.. Kushoto ni mjumbe mwenzake,kutoka mkoani Mwanza, Mussa Ramadhan.
Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (ASP), Deus Sokoni (kulia), akifafanua baadhi ya vifungu vya sheria katika mkutano huo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi, DCP Mohamed Mpinga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano huo ambao ni wanachama wa Chashubuta.
Hapa DCP Mpinga akiagana na wajumbe hao baada ya kufungua mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limesema litavifungia vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya udereva nchini bila ya kuwa na sifa.
Kauli hiyo ameitoa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP) Mohamed Mpinga wakati akifungua mkutano wa pili wa Chama cha Shule Binafsi za Udereva Tanzania (Chashubuta) uliofanyika Dar es Salaam leo.
"Kuanzia sasa Jeshi la Polisi halitasita kukifungia chuo chochote cha udereva kitakachokosa sifa kwani kwa kulea shule mbovu tutaendelea kupata ajali na hivyo kuongeza vifo na majeruhi" alisema Mpinga.
Mpinga alisema kwa mujibu wa sheria ya shule za udereva sura 163 ya 1965 (R.E 2002) mpaka sasa jeshi la polisi limesajili shule za udereva 260 ambazo zitategemewa kutoa madereva bora wenye ueledi wa kutosha kutokana na kuwa chanzo kikubwa cha ajali ni makosa ya kibinadamu ambayo yanafanywa na madereva.
Alisema jeshi hilo litafanya msako nchi nzima kuvibaini vyuo ambavyo havisa sifa na wamiliki wake kuchukuliwa hatua na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria.
Mwenyekiti wa Chashubuta Taifa, Robert Mkolla wakati akisoma risala yao mbele ya Mpinga ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo, alisema moja ya changamoto waliyonayo ni baadhi ya wadau wa sekta ya usafiri na usafirishaji kutoona mchango mkubwa unaofanywa na shule za udereva za watu binafsi wakiamini kuwa vyuo vinavyotoa elimu nzuri ni vile vya serikali pekee.
Post a Comment