PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: CLARA MTOTO ASIYEONA MWENYE NDOTO YA KUWA PROFESA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mtoto Flora Damian mwenye ulemavu wa kutokuona akiwa darasani katika shule ya msingi Patandi ililyopo wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha ....
Mtoto Flora Damian mwenye ulemavu wa kutokuona akiwa darasani katika shule ya msingi Patandi ililyopo wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha .Picha na Ferdinand Shayo

Mtoto Flora Damian mwenye ulemavu wa kutokuona akiwa darasani katika shule ya msingi Patandi ililyopo wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha .Picha na Ferdinand Shayo




Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Kumekua na utamaduni wa baadhi ya watu wenye ulemavu wa aina mbali mbali  kutumia ulemavu wao kama nyezo ya kuwa omba omba lakini kwa mtoto Clara ambaye ni Mwanafunzi wa Darasa la Saba imekua ni tofauti kwani ana ndoto ya kuwa Profesa na kuisaidia jamii yake.

Licha ya hali yake ya ulemavu wa kutokuaona bado ana maono na ndoto za kuwa mtu wa thamani na wa pekee mwenye mchango mkubwa katika jamii yake jambo ambalo linashangaza watu wengi.

Mtazamo wake juu yake mwenyewe umekua ukiwashangaza watu wengi hata walimu wake ,watu wanamuona kuwa haoni lakini yeye anajiona kama Profesa jambo ambalo limenipa nguvu ya kumzungumzia binti huyu.

Clara anajiona na ana maono makubwa  maana yake anaona zaidi ya kuona licha ya ulemavu wa kutokuona alionao lakini bado anaona uwezekano wa kutimia kwa ndoto zake jambo ambalo linawapa faraja wazazi wake,walimu na jamii yake.

Ni moja kati ya watoto ambao wanaamini kuwa kuwa mlemavu si lazima kuwa ombaomba kwani unaweza kuwa mlemavu na bado ukawasaidia hata wale ambao si walemavu.

Ulemavu kwake sio sababu ya kutokuchangia kitu kwenye jamii yake kwani anaamini kuwa anaweza kuwa na mchango chanya utakaoleta mabadiliko kwenye jamii.

Mtoto huyu namfananisha na Steve Wonder mpiga kinanda mashuhuri duniani ambaye haoni na amevunja rekodi duniani ,mtu huyu wanasema kuwa alikua ana macho ya ndani aliona vitu ambavyo wengine hawaoni.

Clara ana  uwezo mkubwa wa kuchambua mambo na kudadisi na hata kupaza sauti kuwatetea wana jamii na watu wenye ulemavu.
Hapa naelezea changamoto zinazowakabili pindi wanapokua shuleni alisema kuwa kumekua na uhaba wa vitabu kwa watoto wasioona  na mashine za kuandikia maandishi yenye nundu ambazo  ni chache na kwa sasa ni mashine tatu pekee  zinafanya kazi .

“Walimu wa elimu maalumu (special education) ni wachache sana ,kuna uhaba wa vitabu vya hesabu na Kiswahili ,tangu nimeanza darasa la kwanza hadi la saba sijawahi kusoma kitabu cha hesabu maalumu kwa wasioona” Alisema Clara

Anaeleza kuwa miundombinu ya majengo ya madarasa pia yamekua si rafiki kwa watoto wenye ulemavu  hivyo anashauri miundombinu ya majengo na shule iendane na mahitaji wa watoto hao.

Clara anasema kuwa ndoto yake ni kuwa Profesa na kuisaidia jamii na taifa lake katika masuala mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.

Mwalimu Mkuu Msaidizi Mbonea Mfinanga ambaye ni Mtaalamu wa Wanafunzi wasioona na Mwalimu wa Somo la Sayansi anasema kuwa Clara ni Mwanafunzi anayeoongoza kwa kufanya vizuri kitaaluma darasani na kuwapita hata wale wasiokuwa na ulemavu.

“Uwezo wa Clara Darasani uko juu sana ukilinganisha na wenzake huwa tunamchanganya na wenzake lakini bado tunaona yuko vizuri” Alisema Mwalimu Mkuu Msaidizi

Mratibu wa Kitengo Cha Walemavu Katika Shule hiyo Mwalimu Shayo amekiri kuwepo kwa upungufu wa walimu na vitabu kwa watoto wenye mahitaji maalumu  na kuiomba jamii,taasisi na serikali kushiriki katika kuboresha maendeleo ya watoto hao ambao wakijengewa misingi bora ya elimu wanaweza kuwa na mchango kwa jamii badala ya kuwa tegemezi.

Mwalimu wa Maarifa ya Jamii anayefundisha katika shule hiyo Marco Mamuya  ameiomba serikali itoe motisha kwa walimu wanaofundisha watoto wenye mahitaji maalumu ili kuongeza ari na hamasa itakayosaidia kupata idadi kubwa ya walimu .
“Tunawaomba wazazi wasiwafiche watoto wenye ulemavu majumbani bali wawalete mashuleni huku waweze kupata elimu ,lishe na mazoezi badala ya kuwafungia nyumbani kwani wanazidi kuwa tatizo licha nya uwezo,vipaji na ubunifu walioanao ambao unaweza kuwasaidia wao na jamii yao” alisema Mwalimu Marco Mamuya

Ferdinandshayo@gmail.com
0765938008

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top