Kituo
cha Mikutano cha KimataifaArusha (AICC)kimemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Daudi Ntibenda madawati 100 yenye thamani shilingi milioni nane ili kupunguza tatizo
la upungufu wa madawati katika mkoa huo.
Akipokea
madawati hayo jijini Arusha jana, Ntibenda amesema kwamba msaada huo ni sehemu ya
juhudi za serikali mkoani Arusha kuwashirikisha
wadau wa maendeleo ili kuhakikisha shule
zote za mkoa huo zinakuwa na madawati ya kutosha.
“Napenda
niishukuru sana AICC kupitia kwa Mkurugenzi Mwendeshaji Elishilia Kaaya kwa kuitikia
vema wito wa serikali ya mkoa wa kuomba wadau wasaidie kuondoa tatizo la upungufu wa madawati katika mkoa
wetu”, alisema Mkuu wa Mkoa.
Alitoa
wito kwa wadau
mbalimbali mkoani Arusha wakiwemo wafanyakazi
wa ofisi ya Mkoa wa Arusha nao kujitokeza ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha
kila mwanafunzi ana kaa katika dawati.
Akizungumza
baada ya kukabidhi madawati hayo, Afisa Mwandamizi waItifakina Uhusiano wa AICC, Catherine Kilinda amesema kwamba AICC
kama shirika la umma linawajibu wakuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha
sekta ya elimu hapa nchini.
“Sisi
kama shirika la umma linalojiendesha kibiashara tunaona fahari kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzaia wa kuhakikisha watoto
wetu wa shule hawakai chini na ndio maana
leo hii tumekabidhi msaada huu ikiwa ni kuunga
mkono juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuinua
sekta ya elimu”, alieleza Catherine.
About Author

Advertisement

Related Posts
- FRIEDKIN CONSERVATION FUND WATOA MILLIONI 84 KUSAIDIA MIRADI YA MAENDELEO KWA JAMII YA MOYOWOSI, UVINZA NA UGALA02 Oct 20180
Baadhi ya wakurugenzi na viongozi wa Friedkin Conservation Fund wakiwa katika maonesho ya na...Read more »
- MOBISOL YASHIRIKI SIKU YA USAFI WA MAZINGIRA DUNIANI, WAHIMIZA MATUMIZI YA NISHATI JUA KUTUNZA MAZINGIRA17 Sep 20180
Baadhi ya wafanyakazi wa Mobisol Wakifanya usafi wa mazingira jijini Arusha mapema leo Baadhi ...Read more »
- JERRY MURRO ATOA MKWARA MZITO KWA WANAARUMERU MARA BAADA YA KUAPISHWA31 Jul 20180
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo katikati akiwa na wakuu wapya wa wilaya za Arumeru Bwana J...Read more »
- WAANDISHI WAWASILI KWA MGANGA WA JADI ILI KUMUELIMISHA JUU YA MADHARA YA UKEKETAJI KWA WATOTO WA KIKE.01 Jun 20180
Waandishi wa redio jamii tano Tanzania toka katika mikoa minne ya Arusha,Manyara,Dodoma na ...Read more »
- WAMAASAI, WASONJO WATAKIWA KUACHA UKEKETAJI01 Jun 20180
Jamii za Kimaasai na Sonjo zinazopatikana katika wilaya ya Ng...Read more »
- WADAU WA UTALII JIJINI ARUSHA WATOA MSAADA KUBORESHA HUDUMA YA AFYA31 May 20180
WADAU wa utalii mkoani Arusha wamekabidhi msaada wa Vitanda 40 kumi &nbs...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.