Jack Wolper Ametoa Somo zuri kuhusu pete ya uchumba wanazovalishwa
wadada na kufungwa nazo...Ameweka picha hii hapa chini na kuandika
maneno yafuatayo
"Trully witchcraft and am sure wanaume wanafanya hivi ili awe na uhakika upo hapo tu unamsubiri wakati yeye anaponda maisha yake
Na mwisho wa siku wengine wanaenda kuoa kwingine sio alikovalisha pete
Binafsi naomba tujitahidi sisi wakina dada (hata mimi najishauri) kutokusimamia ahadi pekee and put your life pending.. You love him COOL
He loves you back EVEN BETTER
ILA ilo lisikufanye ukasimamisha maisha yako kwajili yake... Anataka kukuchumbia kubalianeni whats way forward then Mjipange kwa pamoja kuelekea lengo lenu... Engagement sio one person goal (sio wajibu wa mwanaume pekee kusimamia uchumba wenu na kujua lini utafkia ndoa, ni maisha ya wote wawili na hivi vitu ulizeni hata wazazi wetu VINAPANGWA, vinajadiliwa na vinawekewa kipindi cha kutimiza) mwanzo tamaduni ilikua ni kuchumbia kwa muda tu then ndoa ila siku hizi unaweza parara hata miaka nane na pete mwanaume hana hili wala lile, na sisi kinadada tunavyojua kuachia moyo unakuta maskini hata ukitongozwa unakataa kwakua unajua una mchumba wako.. Unaweka DP ya pete na kumshukuru Mungu... Huku mwenzio anajua ame seal deal anaanza kupeta mtaani na wengine... Si anapata all the benefits.. Tayari ana mke "majukumu" kuna tofauti ya mke wa ndoa na mke wa majukumu..
Utampikia utamfulia utafanya kila kitu ila Mungu pishia mbali akidondoka leo hii itabaki Marehemu alikua hana ndoa wala mtoto... Tena worst ni wale unakuta umeshazaa nao ndo balaa.. Yaani Mungu tunusuru tu sisi waja wako
Kwakweli inabidi wapenzi tubadilike Sio unakubali kupokea lipete la mtu unakaa nalo faithful kumbe mwenzio ana macommitment yake uko anakopajua
Women are strong and we can make it on our own, ndoa ni nzuri na bonus tu
Cha muhimu kupambana usimamishe maisha yako hayo mengine yanakuja tu
Kama kimepangwa imepangwa na kama haijapangwa hata ubinuke haiwezi kua
Ndio maana mimi siku hizi nimejifunza kusugua goti, haya mambo ni Mungu pekee ndio mwenye jibu la mwisho na sahihi.
Lets just pray na kama umeolewa pray for your sisters na hata wanao wa kike..
Kwakweli mahusiano siku hizi yanahitaji Mungu kupita kiasi" Jack Wolper
Post a Comment