Simba ilipomuuza Samatta kwa TP Mazembe ya DR Congo, moja ya masharti ya mkataba ni kulipwa asilimia 20 ya kila anapouzwa lakini hadi sasa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi haijapokea fedha za Genk.
Ili kujiridhisha kabla ya kuchukua hatua zaidi, Simba ilifanya uchunguzi ikiwemo kuwasiliana na Genk na kuhakikishiwa kuwa, tayari waliilipa TP Mazembe fedha zote za usajili.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ameliambia Championi Jumamosi kuwa, walibaini mchezo huo baada ya kuwasiliana na Genk na sasa watalifikisha suala hilo kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
“Kila tukiwasiliana na Mazembe wanasema fedha ya Genk haijaingia kwao, tumewaandikia barua na nakala kwenda Fifa na TFF (Shirikisho la Soka Tanzania), mambo yakizidi tutaenda rasmi Fifa,” alisema Hans Poppe.
Taarifa zinasema Samatta aliuzwa kwa euro 800,000 hivyo Simba inastahili kupata euro 160,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 388.
Chanzo:GPL
Post a Comment