PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: RAISI MAGUFULI KUWEKWA KIKAANGONI NA SERIKALI YA MAREKANI MACHI 28
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Marekani imezidi ‘kuikalia kooni’ Serikali ya Rais John Magufuli baada ya Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) la nchi hiyo kua...


Marekani imezidi ‘kuikalia kooni’ Serikali ya Rais John Magufuli baada ya Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) la nchi hiyo kuamua kukutana tena Machi 28 kuijadili Tanzania.

Marekani ilisitisha kutoa msaada wa dola milioni 472 (Sh. trilioni 1) za awamu ya pili ya fedha za maendeleo kutoka MCC Disemba 16 mwaka jana, baada ya Tanzania kushindwa kutimiza maagizo waliyopewa na bodi hiyo.

Awali, katika angalizo lake kwa serikali ya Magufuli iliyoingia madarakani Novemba 5 mwaka jana, MCC ilitaka kupatiwa ufumbuzi mkwamo wa kisiasa wa Zanzibar na pia kupatiwa ufafanuzi kuhusu watuhumiwa waliokamatwa kwa makosa ya mtandao wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.

Ilifahamika kuwa maelekezo ya MCC kwenda kwa mamlaka mbalimbali za serikali ya Tanzania, yalionyesha kuwa lipo tishio la kufutwa kwa msaada huo (trilioni moja) iwapo mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar uliotokana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi, usingekuwa umepatiwa ufumbuzi.

MCC pia ilitaka kutolewa ufafanuzi wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, kabla ya kikao cha bodi ya MCC mwezi De67semba mwaka jana.
Kwa mujibu wa ratiba ya MCC, kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kitakutana Machi 28 kupitia agenda sita, Tanzania ikiwa ni ajenda ya tano inayotarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo.

Katika kikao hicho, Tanzania itajadiliwa kama itakuwa na hadhi ya kuendelea kupokea misaada zaidi kutoka MCC, baada ya msaada wa awali kusitishwa.

Mkutano huo unatarajiwa kuendelea kuipa kibano Serikali ya Rais Magufuli kwani uchaguzi wa marudio unaofanyika kesho umesusiwa na chama kikuu cha upinzani cha CUF kinachodai kushinda Oktoba 25.
Matokeo ya uchaguzi huo yalifutwa na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, Jecha Salum Jecha, kwa madai ya kukiukwa kwa taratibu nyingi za uchaguzi.

YATAKAYOJADILIWA NA BODI MCC
Baadhi ya mada zitakazojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na kupitia hadidu za rejea za kikao kilichofanyika Desemba 16, mwaka jana cha mkutano wa kamati ya ukaguzi, mrejesho kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu, Tanzania, namna bora ya kupambana na umasikini na mrejesho kuhusu mradi wa maji wa Jordan.

Tofauti na fedha zinazotolewa na wafadhili wengi duniani, fedha za MCC hazitakiwi kurudishwa na nchi inayopewa fedha. Aidha, nchi husika hupewa uhuru wa kuchagua aina ya miradi ya maendeleo ambayo inataka igharimiwe na fedha hizo.

Katika fedha za awamu ya kwanza za MCC, Tanzania ilipata dola milioni 698 (Sh.trilioni 1.46), ambazo tayari zimesaidia kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ya barabara na usambazaji wa umeme vijijini.

KAULI YA KATIBU MKUU HAZINA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile, alipoulizwa kuhusu hali hiyo, alisema hawezi kulizungumzia suala la uchaguzi wa Zanzibar kwa kuwa uchaguzi unafanyika kesho.

Kuhusu Sheria ya Makosa ya Mtandao, alisema Sheria hiyo ni halali kwa kuwa ilipitishwa na Bunge ambalo ndicho chombo cha uwakilishi wa wananchi.

Alisema hakuna nchi duniani ambayo haijiwekei tahadhari ya kiusalama hivyo aliwataka Watanzania waitetee nchi yao na kuikubali Sheria hiyo.

“Kuhusu Zanzibar nadhani hata wewe unajua kuwa uchaguzi unafanyika keshokutwa (kesho), hivyo sina cha kukomenti ila ninachotaka kusema kuwa ni sheria hii ilitungwa kwa dhumuni la kuilinda nchi, hivyo kila Mtanzania anawajibu kuipokea Sheria hii,” alisema Likwelile.

Kama MCC watakutana Machi 28, alisema, serikali itasubiri kuona nini kitadajiliwa na kutolewa

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top