PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAKALA: USIUE NDOTO YAKO KWASABABU YA PESA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Na Ferdinand Shayo,Arusha. Kila mtu duniani ana ndoto haijalishi ni ndoto gani unayo ,ndoto uliyonayo ina thamani kubwa kuli...



Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Kila mtu duniani ana ndoto haijalishi ni ndoto gani unayo ,ndoto uliyonayo ina thamani kubwa kuliko fedha kuliko kitu chochote kile,Ndoto uliyonayo ina nguvu kubwa ya kubadilisha maisha yako na kukufikisha sehemu ambayo ulitaka ufike ama zaidi ya pale ulipotarajia kufika.

Ndoto yako inaweza kukupeleka sehemu mbalimbali duniani ukazunguka kufanya mambo yako si kwa sababu una fedha sana ni kwa sababu una ndoto ni vyema utambue nguvu ya ndoto uliyonayo ni kubwa sana kuliko fedha.

Ndoto inaweza kuzaa fedha kwa maana matunda ya ndoto zako yanaweza kuwa fedha  ila fedha haiwezi kuzaa  ndoto hivyo ndoto ni kubwa kuliko fedha.

Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa mtu masikini kuliko wote duniani ni Yule asiyekuwa na ndoto hivyo utakubaliana nae kuwa kila mwenye ndoto ni tajiri na si masikini tena maana ana kitu cha thamani na cha pekee  na cha tofauti ambacho  hamna mwenye nacho usipokua wewe.

Tatizo kubwa ni kwamba watu wengi wameua ndoto zao kwa kisingizio cha kukosa fedha iwe   kidogo au kubwa  maana hakuna pesa inayozidi ndoto ila ndoto zinazidi fedha.

Tatizo lingine ni watu wengi hawajui kuwa ndoto zao zina nguvu kubwa kufanikisha maisha yao kijamii,kiuchumi ,kisiasa na kila Nyanja ya maisha kulingana na ndoto yao ilivyo .

Ndani ya ndoto zako kuna kila kitu unachokitaka kuna kila kitu unachokihitaji iwe ni fedha ,utajiri,umaarufu,familia nzuri,mume mzuri ,mke mzuri,watoto wazuri,kazi nzuri,afya nzuri ivyo ukiacha kutafuta fedha ukatafuta kutimiza ndoto zako utapata kila kitu unachokitaka ikiwemo utoshelevu na amani ya moyo ,peace of mind.

Tatizo lipo kwenye kufanya ndoto zako zitokee ziwe katika uhalisia zikuzalie mafanikio,haijalishi una ndoto kubwa kiasi gani kama hautaitimiza ikaja kwenye uhalisia ikakuzalia mafanikio uwe na uhakika utakufa masikini ukiwa na utajiri wa ndoto jambo ambalo linaumiza na linatesa maisha ya watu wengi wanaishi maisha ya chini ya kiwango ambacho walitakiwa kuishi kulingana na ndoto zao.

Kiwango cha maisha unayoishi kinatakiwa kilingane na kiwango cha ndoto uliyonayo haiwezekani una ndoto kubwa alafu unaishi maisha madogo ,inasikitisha .Ndoto yako ndo imebeba kusudi la maisha yako kama utaishi katika ndoto yako maana yake utakua hujaishi maisha yako maana maisha yako halisi yako kwenye ndoto zako.

Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa watu wengi duniania hawaishi bali wapo kunatofauti kati ya kuishi na kuwepo,kuishi ni kutimiza ndoto zako na kuishi ndani ya kusudi la maisha yako ila kama hautimizi ndoto zako uko nje ya kusudi la maisha yako maana yake wewe hauishi bali upo ,ama upo upo kama uliwahi kusikia mtu anauliza vp mzima wewe anajibu mimi nipo nipo yani ni kama ananing`nia angani hana anachosimamia hana anachotazamia anaishi kama bendera fata upepo .

Anaamka asubuhi kwa sababu watu wanaamka ukimuuliza kwanini umeamka anasema ni kwa sababu watu wameamka hana sababu za msingi,kataa kuishi bila agenda ,bila kuwa na ndoto ambayo kila siku unapiga hatua kuifikia ama uko ndani yake sasa katika kuitimiza na kuifanikisha kwa kiwango cha juu.

Kila kitu kipo kwenye ndoto zako tafuta kutimiza ndoto zako kuliko kutafuta fedha na kuacha ndoto zako kwa sababu pesa ni moja kati ya bidhaa iliyoko ndani ya ndoto zako.

Sisemi watu wasitafute pesa  wazitafute tena kwa bidii ila wasisahau  kutafuta kutimiza ndoto zao na kutumia pesa zao kama moja kati ya nyezo za kuwawezesha kutimiza ndoto zao maana hata maandiko yanasema kuwa pesa ni nguvu.

Ukweli ni kwamba pesa sio kila kitu pesa huwa hazitoshi na zinaweza zisitosheleze hata kama ni nyingi kiasi gani kama unabisha waulize matajiri kama wamewahi kuridhika lakini katika kutimiza ndoto zako kuna utoshelevu kiasi na kuridhika kiasi Fulani (satisfication) hata kama si kwa asilimia 100% .

Mwandishi Mashuhuri wa Vitabu Myles Munroe aliwahi kusema kuwa “Watu wenye  kusumbuliwa na msongo mkubwa wa mawazo ni wale ambao ndoto zao hazijatokea kwenye uhalisia zinawasumbua”

“Most frasturated people are these people who they are dream are not come to the reality” Myles Munroe

Inawezekana unasumbuka sana kwenye maisha yako kwasababu hujatimiza ndoto zako maana ndoto huwa haimwachi mtu akatulia inampa mahangaiko,mfadhaiko wa kutaifuta kuiachilia iyo ndoto iliyoko ndani yako inataka kutokea kwenye uhalisia duniani kwa faida yako na jamii yako.

Kuwa na ndoto ni kama ujauzito ambao kila mtu anakua  nao haijalishi ni mwanamke au mwanamke na anatakiwa azae icho kitu kilichoko ndani yake iwe ni kipaji cha mziki  mzuri,vitabu,ubunifu na uwezo Fulani uje kwe uhalisia.

Hivyo kila mtu anapaswa azae ,ndoto yako izae ,uwezo ulionao uzae unaweza kukuzalia mafanikio makubwa usikubali kufa na kitu cha tahamani kilichoko ndani yako kilete duniani kitoe kilete mabadilko .

Hakuna ndoto kubwa wala ndoto ndogo fikiria mtu aliyegundua lipstick mafuta ya kupaka mdomoni leo hii wanawake dunia nzima wanapaka lipstick si jambo dogo hata kidogo.

Hujaja duniani kuwa mtu wa kuhangaikia fedha ,inatakiwa fedha ikuhangaikie wewe ,pesa ikupende na ikutamani na si wewe utamani fedha maana tamaa ya fedha ni mbaya inazaa uovu na uasi wakati mwingine.

Tengeneza miundombinu ya pesa kukufikia na hiyo miundombinu iko kwenye ndoto  zako ,maono yako,kipaji chako na uwezo ulionao.

Kwenye  ndoto zako Kuna ramani na barabara za watu kupita kukuletea fedha kutokana na kile ulichonacho,kile ulichonacho ni cha thamani sana.

Kile ulichonacho ni kikubwa zaidi ya fedha ,tafuta kukitimiza hicho ulichonacho ,anza sasa uwezo unao nguvu unayo.

Katika kutimiza ndoto zako usikubali kuzuiwa na fedha,mazingira ,mtazamo hasi,marafiki,jaribu kuwa mtu asiyezuilika ili uweze kuzifikia ndoto zako.


0765938008

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top