Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Wiki mbili
zilizopita katika maadhimisho ya wiki ya sheria ,Rais John Pombe Magufuli
alitangaza kuwa nchi imejipanga kuanzisha mahakama ya kushughulikia mafisadi na watu wanaohujumu uchumi wa nchi haiukupita
hata mwezi Vigogo waliokua wakishukiwa kuisababisha hasara serikali ya bilioni
11 na matumizi mabaya ya madaraka Basil
Mramba na wenzake wakasomewa hukumu ya kutumikia kifungo cha nje jambo ambalo
watanzania wengi wamelitafsiri kama mzaha uliofanyika mbele ya Rais na
Watanzania ambao wako siriaz wanataka waone kazi.
Hukumu hiyo
ya mahakama imetoka katika muda muafaka ambayo Tanzania ina Rais anayesifika
kuwa ni kiboko ya mafisadi na mchapakazi .
Watanzania
hawaoni nia ya dhati ya Rais kupambana na ufisadi kufuatia hukumu hiyo licha ya
mambo aliyoyafanya hapo nyuma ya kuibua ufisadi wa Bandarini ,madudu ya
Muhimbili na TRA.
Huenda kwa
kasi ya Rais na hukumu iliyotolewa inaonyesha kuwa huenda kukawa na kidhibiti
mwendo cha Rais wetu mpendwa ambaye Watanzania wengi wana imani nae.
Mbaya zaidi
ni kufuru wanayoifanya kina Mramba wako kifungoni na bado wanaoengea na vyombo
vya habari na kuitaka serikali itoe vifungo vya nje ili kupunguza gharama kubwa
za chakula na matibabu .
Nani anawapa
kiburi watu hawa ambao wanatuhumiwa kuhujumu uchumi wa nchi jambo ambayo ni la
aibu bila aibu wanaongea na Waandishi wa Habari na kutolewa kurasa za mbele
kama vile MRAMBA AFUNGUKA.
Wanataka
kutonyesha nini kwa kuongea sana kwamba serikali ni dhaifu zaidi ama haina meno ama
wao wako juu ya sheria ,ama wanaweza kuzichezea sheria kama wanavyotaka.
Labda mfumo
wa kimahakama bado haujajiandaa kupambana na ufisadi na watu wanaoihujumu nchi
hii yenye matatizo kede kede yenye vilio kila kona vya umasikini ,kukosa huduma
za afya,maji,nishati na elimu bora.
Mapambano
dhidi ya ufisadi na rushwa bado yanaonekana kama mchezo wa kuigiza kwasababu tu
ya huu mfumo wa kulindana ambao unazidi kuitafuna nchi hii ambayo mwisho
itabaki mifupa.
Kwa mwendo
huu uchumi utakua kwenye mikono ya watu wachache na umasikini utaongezeka kwa
watu wengi.
Mtindo huu
wa kina mramba utaendelea kuigeuza Tanzania kuwa shamba la bibi kila mtu
anafanya atakalo na hakuna wa kumzuia .
Itafika
mahali viongozi hawatakua na ujasiri wa kupinga ufisadi wala kuuekemea maana
ufisadi utakau umetamalaki.
Ilifika mahali
watu wakafikiri kuwa hadi ikulu imejaa
wasoma ramani jambo ambalo linashusha imani ya wananchi kwa serikali yao.
Lakini kwa
hii awamu ya Magufuli watanzania bado wana imani nayo ikitokea suala linguine kama
la Mramba na yanayofanana na hayo
Watanzania watajikatia tama kwa kweli.
Tunahitaji
kuona commitment ya kuondoa ufisadi ,dhamira ya kweli sio kutoa matamko makali
alafu ukirudi ndani unafyata mkia .
ferdinandshayo@gmail.com
0765938008
0765938008
Post a Comment