Home
»
HABARI ZA AFYA
» DK. KIGWANGALLA AUPA MIEZI SITA UONGOZI WA HOSPITALI YA RUFAA MOROGORO KUREKEBISHA MFUMO WA CHUMBA CHA UPASUAJI
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro mapema jana Februari 16 na kubaini matatizo mbalimbali ikiwemo chumba cha upasuaji, mfumo wa malipo na ubovu wa vifaa vya maabara.
Dk. Kigwangalla ametoa siku 60 vifaa ndani ya chumba cha upasuaji ziwe zimerekebishwa huku akiagiza ndani ya miezi sita mfumo wa chumba cha upasuaji uwe umetengenezwa vizuri na endapo watashindwa basi atachukua hatua za kufungia vyumba hivyo vya upasuaji kwani vikiendelea kuachwa hivyo vitaendelea kusababisha matatizo Zaidi kwa wanaopaatiwa huduma.
Dk. Kigwangalla akiwa ameambatana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Ritha Lyamuya walitembelea vitengo kadhaa ikiwemo chumba cha upasuaji, jengo la maabara, pamoja na majengo mengine ikiwemo lile la wamama wajawazito na jengo maalum la daraja la kwanza (Grade A).
Hata hivyo ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kushughulikia mara moja mapungufu yaliyobanika. Katika jengo la kuhudumia wagonjwa wa daraja la kwanza, Dk. Kigwangalla alikuta hali ya uchafu na muonekano usiofaa kwa matumizi ya kuitwa daraja la kwanza.
Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, awali lawama nyingi zinatupiwa Wizara yake wakati ukweli ni kuwa Hospitali zipo chi ya Wizara ya TAMISEMI ambao wanashughulikia huku wao Wizara ya afya wakisimamia baadhi ya mambo ikiwemo ukaguzi, madawa, mashine na vifaa.
About Author

Advertisement

Related Posts
- WADAU WA UTALII JIJINI ARUSHA WATOA MSAADA KUBORESHA HUDUMA YA AFYA31 May 20180
WADAU wa utalii mkoani Arusha wamekabidhi msaada wa Vitanda 40 kumi &nbs...Read more »
- WAZIRI UMMY MWALIMU: RMO,DMO TENGENI SIKU ZA UCHUNGUZI WA SARATANI29 Apr 20180
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza leo Jijini Tan...Read more »
- Rekodi ya Madaktari Wanaomtibu Tundu Lissu Ubelgiji Usipime Kabisa, wanategemewa na bara zima la ulaya20 Mar 20180
Rekodi ya Madaktari Wanaomtibu Tundu Lissu Ubelgiji Usipime Kabisa HUU ndio...Read more »
- WAZIRI WA AFYA AKIRI CHANGAMOTO YA UHABA WA MADAKTARI17 Jan 20180
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jin...Read more »
- TABIA ZA KUEPUKA ILI UWE MWENYE AFYA BORA19 Dec 20170
Na Jumia Food Tanzania Chakula huupatia mwili virutubisho ili uweze kufanya kazi kwa ufasah...Read more »
- PITIA HAPA UFAHAMU FAIDA MBALIMBALI ZA TANGAWIZI KATIKA MWILI WA BINADAMU04 Dec 20170
Hicho ni kiungo kinachotokana na mzizi wa mmea unaoitwa Tangawizi. Ni mmea unaofanana sa...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.