Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo Jumapili ya February 7 kwa michezo 7 kupigwa katika viwanja tofauti, klabu ya Dar Es Salaam Young African ambayo ilikuwa mikoani kucheza mechi zake mbili za muendelezo wa raundi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2015/2016, imerejea kucheza mchezo wake 18 dhidi ya JKT Ruvu.
Yanga waliingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kuponea chupuchupu kufungwa na Tanzania Prisons katika mchezo wake uliopita, baada ya kuambulia kutoa sare ya kufungana goli 2-2, Yanga waliingia uwanjani wakiwa hawataki kurudia makosa, kwani dakika ya 12 Simon Msuva alifanikiwa kufunga goli la uongozi kwa Yanga.
Neema ya magoli kwa Yanga iliendelea baada ya mshambuliaji wao wa kimataifa kutoka Niger Issofou Boubacar kupachika goli la pili dakika 2 kabla ya kwenda mapumziko, kipindi cha pili Yanga walirejea uwanjani na kufanya mashambulizi mengi lakini walifanikiwa kutumia nafasi mbili kwa Donald Ngoma kupachika goli la tatu dakika ya 63 na Simon Msuva kufunga goli la nne na kufanya mchezo, umalizike kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 4-0. Yanga wanaendelea kukaa kileleni kwa kutimiza point 43 wakifuatiwa na Simba kwa tofauti ya point 1.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa February 7
- Kagera Sugar 0 – 1 Simba
- Mbeya City 0 – 0 Tanzania Prisons
- Ndanda FC 1 – 1 Mtibwa Sugar
- Azam FC 1 – 0 Mwadui FC
- Toto Africans 2 – 1 Coastal Union
- Majimaji FC 1 – 0 Mgambo JKT
Post a Comment