Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro Eng. Dorothy Ntenga
akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa namna maji yanavyopiga kingo za daraja la Dumila wakati Waziri
huyo akikagua ujenzi wa kingo mpya zinazojengwa kudhibiti mafuriko hayo.
Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng. Leornad Chimagu
(kulia),akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa kuhusu athari za mafuriko katika kingo za
barabara ya Gairo-Dodoma eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma.
Muonekano
wa Daraja la Dumila mkoani Morogoro lilivyo sasa kufuatia mvua
zinazonyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kusababisha mafuriko
yanayoelekea katika Mto Mkondoa.
Mafundi
wakiendelea na ujenzi wa kingo za barabara zilizo athiriwa na mvua
zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kusababisha
uharibifu wa barabara katika eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia),
akitoa maelekezo kwa Meneja wa TANROADS mkoa wa Dodoma Eng. Leornad
Chimagu kuhusu ujenzi wa kingo za barabara hiyo kabla hazija athiri
huduma za usafirishaji.
Mafundi
wakiendelea na ujenzi wa kingo za barabara zilizo athiriwa na mvua
zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kusababisha
uharibifu wa barabara katika eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma.
Magari
yaliyoegeshwa katika kingo za barabara yanavyochangia uharibifu wa barabara na
kusababisha ajali, hili ni eneo la Kibaigwa mkoani Dododma.
****************
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemwagiza Meneja wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu kuhakikisha ukarabati wa barabara katika eneo la
Kibaigwa unaanza jumapili.
Profesa
Mbarawa ameyasema hayo alipokuwa akikagua athari za uharibifu wa barabara
zilizosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Iringa –
Dodoma na kusababisha mafuriko yanayoharibu kingo za barabara.
“Hakikisheni
Jumapili kazi ya ujenzi hapa inaanza na ikamilike kwa muda mfupi ili kutoathiri
huduma ya usafiri katika barabara hiyo kutokana na umuhimu wake”, alisema Prof.
Mbarawa.
Waziri
Mbarawa amewataka TANROADS washirikiane na Kikosi cha Usalama Barabarani kudhibiti magari
yanayoegeshwa katika maeneo yasiyo rasmi na hivyo kusababisha ajali na
uharibifu wa barabara hususani katika maeneo ya Dumila mkoani Morogoro na
Kibaigwa mkoani Dodoma.
Mapema
Waziri Mbarawa alikagua ujenzi wa kingo za barabara unaoendelea katika eneo la
Dumila mkoani Morogoro ambapo amemuagiza Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro
Eng. Dorothy Ntenga kuhakikisha ujenzi huo wa kudhibiti barabara na daraja la
Dumila unakamilika kabla ya Februari 15 ili kukabiliana na mafuriko wakati wa
mvua za masika zinazokaribia kuanza.
“Chimbeni
mchanga kwenye mto ili kuwezesha maji kupita kwa urahisi na kuondoa tishio la
mafuriko yanayo athiri daraja hilo wakati wa mvua za masika”, alisisitiza
Waziri Mbarawa.
Naye
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro, Eng. Dorothy Ntenga amesema ili kudhibiti
mafuriko katika eneo la Dumila juhudi zinaendelea kupunguza mchanga na hivyo
kuwezesha kupita maji kwa urahisi.
Profesa
Mbarawa alikuwa katika ziara ya kukagua athari za mafuriko katika barabara ya
Morogoro-Dodoma ambapo maeneo ya Dumila na Kibaigwa yameathirika zaidi.
Post a Comment