Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Wahitimu wa
vyuo vikuu nchini wametakiwa kuondokana na dhana ya kuajiriwa na badala yake wawe wabunifu na kutengeneza ajira zitakazosaidia kupunguza tatizo sugu
linalowakabili wahitimu wengi.
Hayo yameelezwa na Dokta Godwin Lekundayo ambaye ni Askofu wa kanisa la
Waadventista Wasabato kanda ya kaskazini mwa Tanzania alipokua akihutubia katika
mahafali ya tisa ya chuo kikuu cha Arusha
yaliyofanyika chuoni hapo,Askofu
huyo alisema kuwa kutokana na ugumu ulioko kwenye soko la ajira wahitimu hawana
budi kufikiria kujiajiri.
Askofu Godwin alisema kuwa kutokana na ufinyu wa nafasi za
ajira serikalini na sekta binafsi wasomi
wanapaswa kuamka na kufikiria kujiajiri
zaidi kuliko kuajiriwa .
``najua kujiajiri
kunahitaji mitaji, ila ni vyema kufanya hivyo ili kurahisisha maisha yetu, ya
jamii, na kuondokana na mawazo ya kuajiriwa tu, kwa kuwa soko la ajira ni gumu
kwa sasa.`` alisema askofu huyo.
Makamu mkuu wa chuo hicho Profesa,
Emmanuel Matiku aliwataka wahitimu kutumia elimu zao vizuri kwa kuwasaidia
wazazi waliowasomesha ili kuwakwamua katika umasikini kwa kuwa wamejifunga
mkanda kuhakikisha wanao wanasoma na kuhitimu masomo yao.
``elimu
mliyopata msiitumie kwa faida zenu binafsi, zitumieni kuwakwamua wazazi katika
umasikini, na kuielimisha jamii yote`` Alisema Makamu huyo
Kiongozi wa wanafunzi waliohitimu
Bw Jackson Elias kwa niaba ya wanafunzi wengine aliusihi uongozi wa chuo kikuu
cha Arusha kuendelea kutatua kwa wakati changamoto wanachuo ikiwemo suala la
mikopo ili kuwawezesha wanachuo waliopo kusoma kwa furaha kama walivyosoma wao.
Zaidi ya wahitimu 1,000 walihitimu
katika ngazi ya astashahada, stashahada na shahada kwenye fani mbalimbali
ikiwemo elimu, biashara na lugha.
Post a Comment