Na Godrich
Izack,Arusha.
Leo tarehe 9/12/2015 nimeiona Tanzania
kwa namna tofauti sana na nimepata wasiwasi mkubwa sana. Ni baadhi ya vitu
ambavyo binafsi nilichagua kupambana navyo katika maisha yangu binafsi na jamii
yangu kwa ujumla.USAFI!.Usafi akili,mwili na roho.Namaanisha usafi kuanzia
ndani mpaka nje,tena kwa mtu moja moja kwanza na baade jamii nzima.
Tangu Raisi John Pombe Magufuli
aingie madarakani amefanya alivyoweza,pongezi sana kwake pamoja na waziri mkuu
Mh.Mjaliwa. Nilichojifunza kwa Dr.JPM ni kwamba sababu yeye ni mchapa kazi,mtu
wa kufanya vitu vitokee na mtu anayesimamia vitu anavyoamini,aligundua kwamba
tatizo ni watu wake anaowaongoza,watu wavivu,wazembe,wachafu,watu wanaotaka
kuambiwa fanya hivi au usifanye,watu wasiofikiria nje ya box,yaani ni watu wa
hivi hivi (people like this like that). Ninachokiona hapa ni kwamba raisi bado
anakazi kubwa sana kwa aina ya watu anaowaongoza. Yote hii imetokana na mifumo
ya uongozi iliyopita na mifumo ya maisha mabovu ya vizazi vilivyopita,mifumo inayoendelea
kutafuna kizazi cha sasa.
Nimesikitika sana kuona watu
wakifanya usafi sehemu ambazo walikua wanaishi kila siku,wanafanya kazi hapo kila
siku, wanalala hapo hapo, wanakaa na familia zao, lakini mpaka waambiwe wafanye
usafi ndio wafanye!huo ni upumbavu na uzembe wa hali ya juu. Eti watu wasomi, tena
ni watu waheshima kabisa tena wenye umri kuliko hata raisi lakini kufikiria
kwamba wanapokaa nipachafu na wanatakiwa wapasafishe wameshindwa. Naona ni
maajabu mengine tena funga mwaka. Cha kushangaza ni kwamba nawasikia wanafurahia
kabisa nakusema eti “inawezekana”,Doh!sasa nashangaa kilichokua kinawashinda ni
nini?
Nimegundua kwamba kumbe uchafu
sio tu kwenye mazingira yanayotuzunguka ambayo asilimia 100% sisi wenyewe ndio
wazalishaji wakubwa wa taka hizo tena kwa kutokufikiria sawasawa. Uchafu mkubwa
na mwingi sana upo katika fikra za hawa watu kwa sababu kinachoonekana nje ni
matokea ya kilichokua na kukomaa ndani.Watanzania wengi ni wachafu wa
fikra,tena uchafu uliokithiri ambayo matokeo yake ndio uzembe, uvivu, uchafu wa
mazingira, ujinga, elimu mbovu, wizi, uchoyo, rushwa, matatizo ya ajira,
umaskini uliokithiri, ufisadi na kutowajibika sawasawa ambavyo vyote kwa pamoja
vinapelekea kuchelewa kwa maendeleo ya Nchi hii yenye kila aina ya utajiri.
Inashangaza sana kuona watu
wakifukua mitaro ambayo kila siku iko hapo hapo wanapokaa na inapitisha maji na
saa nyingine yanakwama hapo mpaka watu wanaugua kipindupindu lakini eti walikua
hawaoni kama panatakiwa kuzibuliwa au kufanywa namna maji yapite kwa urahisi.huu
si upumbavu sasa!
Watu wa kuambiwa fanya hivi au usifanye hivi wapo wengi sana ni mzigo
katika kila sekta na katika nchi nzima kwa ujumla wake, na ndio hao wajanja
wajanja waotimuliwa kazi na Raisi kwa aibu kwa sababu ya uchafu wao.Wengine ni
kulalamika tu hakuna ajira,wako na mavyeti tu wakilalama sasa najiuliza mbona
leo watu wanafanya kazi? inamaana
walishindwa kuona hizo fursa kwa sababu ya upofu na uchafu uliosheheni katika
fikra zao.
Kama tu kufanya usafi wa maeneo
yanayowazunguka, wanapofanyia kazi wameambiwa unafikiri ni vitu vingapi
hawafanyi mpaka waambiwe?Unauhakika gani vitu walivyofanya hapo awali kabla
hawajaambiwa na Raisi kama walifanya sawasawa na ilivyotakiwa?Vipi wale
wakandarasi wenye tenda za usafi katika majiji na manispaa nini wanafanyaga?chemba
za idara ya maji zinazofanyiwa usafi leo je? Kumbe kutokomeza malaria, kipindupindu
na magonjwa mengi tu inawezekana kabisa?
Nadhani tunahitaji usafi wa fikra
na akili zetu kwanza.
Godrich Izack
Post a Comment