Taarifa kutoka mjini Morogogoro zinaeleza kuwa sherehe hizo nusura zivunjike baada ya kutawaliwa na majonzi kwa hali ya juu huku baadhi ya wahudhuriaji wakidondosha machozi kutokana na maelezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa vyama hivyo.
Mmoja kati ya waandaaji wa sherehe hizo, Bi. Bertha Kombe alieleza katika sherehe hizo kuwa vijana wengi walitupa kadi zao za kupigia kura baada ya matokeo ya urais huku afya za akina mama wa chama hicho zikidhoofu kutokana na kutoridhishwa na muenendo wa uchaguzi huo.
“Vijana wengi mitaani wamevunjwa mioyo na kutupa shahada zao za kupigia kura, kina mama tumejikuta tukikonda na kushindwa kula kwa sababu tunatumia muda mwingi kutafakari kilichotokea,” alisema Bi. Kombe.
Viongozi wa Chadema waliwashukuru wananchi kwa kuitikia wito na kuwataka kuanza harakati za kuomba kura kwa ajili ya mwaka 2020.
Post a Comment