PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: BODI YA LIGI KUFANYA SEMINA NA UONGOZI WA FDL.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
N A; YOHANA CHALLE. ARUSHA. Ofisa mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Boniface Wambura amesema kuwa Timu za Ligi daraja la kwa...


NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.

Ofisa mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Boniface Wambura amesema kuwa Timu za Ligi daraja la kwanza zinatakiwa kujirekebisha mapema kabla ya mzunguko wa pili kuanza.

Wambura Alisema hayo jijini Arusha alipohudhulia mchezo wa ligi daraja la kwanza kati ya JKT Oljoro na Polisi Tabora, huku akiwa anasisitiza kuwa ligi hiyo itaanza kuoneshwa kwenye Televisheni pindi mzunguko wa Pili utakapoanza, hivyo kuna baadhi ya makosa yanaonekana ambayo sio sahihi kwa Timu za ligi daraja la kwanza kuzifanya.

“Nimefanya uchunguzi kwenye michezo kadhaa ya ligi hii na nimegundua dakika za mwisho waokotaji wa mipira (Ball Boys) wanakuwa wameshaondoka jambo ambalo sio sahihi,kwa kuwa wanatakiwa kuondoka uwanjani pindi mchezo unapoisha”alisema Wambura.

Aliongeza kuwa kuna vitendo ambavyo havifai kufanywa kwenye mchezo, kwa kuwa ni kinyume na taratibu na sheria za kisoka kwa kuwa zinashusha hadhi ya timu na ligi pia, japo timu husika inaamini inasaidia kupoteza muda.

Wambura alisema kuwa Timu nyingi za ligi daraja la kwanza hazina uhamasishaji, tofauti na zile zilizokuwa ligi kuu, hivyo Bodi ya ligi imejiandaa kukaa na viongozi wa timu ili kuliangalia suala hilo kabla ya kipute cha mzunguko wa pili kuanza.

“Wasiitazame TFF au ya Bodi ya ligi, unapokuwa mwenyeji katika mchezo unatakiwa ufanye uhamasishaji ili watazamaji waje kwa wingi kwa kuwa mapato yanayopatikana uwanjani wenyeji ndio wanaopata asilimia kubwa ya mapato kuzidi mgeni”.

“Mwezi ujao tunatarajia kufanya semina na maofisa Habari na maofisa masoko wa timu zote zinazoshiriki ligi daraja la kwanza ili tuwasaidie jinsi ya kupata wadhamini watakaowaidia katika timu zao” alisema Wambura.

Wachezaji na watazamaji wamekumbushwa kuzingatia sheria za michezo hasa kwenye michezo inayohusisha timu za Jeshi au Polisi zimeonekana kuvunja Sheria kila wakati jambo ambalo sio zuri kwa wanamichezo.
 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top