PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: AFC YANASA WATATU WAPYA, YAONGEZA KOCHA.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE ARUSHA. Timu ya AFC ya jijini hapa ambayo inajiandaa na kushiriki ligi daraja la pili ngazi ya Taifa (SDL), Ime...

NA; YOHANA CHALLE
ARUSHA.

Timu ya AFC ya jijini hapa ambayo inajiandaa na kushiriki ligi daraja la pili ngazi ya Taifa (SDL), Imeongeza kocha na wachezaji wapya ili kuimalisha zaidi kikosi hicho ambacho ni kipenzi kikubwa cha wakazi wa Arusha.

 Akizungumzia hilo katibu msaidizi wa timu ya AFC, Charles Mwaimu alisema kuwa tayari wameongeza wachezaji watatu ambao ni Athuman Ponda, Abdallah Kidula na Amour Hamad.

Huku Kocha atakayekinoa kikosi hicho ni Mussa Rashid Omari aliyekuwa kocha wa timu ya Bishop Durning.

“Hatuhitaji lawama kwa sasa tumefanikiwa kumpata kocha mahili ambaye ni Mkazi wa Arusha na Mpenzi wa AFC na wachezaji watatu, mmoja kutoka Tanga, mwingine Dar es Salaam na wa tatu kutoka Zanzibar” aliesma Mwaimu.

Aliongeza kuwa Athuman Ponda alikuwa mchezaji wa Coastal Union Miaka ya nyuma ila kwa sasa alikuwa anafanya mazoezi na timu ya Villa Squad ya Dar es Salaam baada ya kukosa timu kwa muda mrefu.

Alisema kuwa wachezaji wote wameshaingia kambini mpaka hivi sasa na hakuna majeruhi, isipokuwa Martin Teobard aliyepata matatizo ya kifamilia hivyo yupo kwao Mkoani Morogoro na ifikapo jumatatu atakua amesharudi kambini kuendelea na mazoezi.

Hadi sasa kikosi cha AFC kinafanya mazoezi na marafiki zao wakubwa kikosi cha JKT Oljoro inayoshiriki Ligi daraja la kwanza hivyo hiyo ni faida kubwa kwa timu ya AFC kujua mapungufu yao kabla ya SDL kuanza.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top