NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Timu
ya AFC inayojiandaa na ligi daraja la pili ngazi ya Taifa (SDL),
imeshaingia kambini na kuanza mazoezi kwa siku mara mbili ili
kujiimarisha vilivyo kuelekea katika ligi hiyo inayotarajia kuanza
kutimua vumbi mwanzoni mwa mwezi ujao.
Katibu
msadizi wa Timu hiyo Charles Mwaimu alisema kuwa tayari timu hiyo
imeshaingia kambini tangu wiki iliyopita huku ikifanya mazoezi mara
mbili kwa siku katika Dimba la Sheikh Amri Abeid.
“Timu
ipo kambini Huko Oljoro ikiwa na kikosi cha wachezaji 22 tangu wiki
iliyopita na tunafanya mazoezi pamoja na JKT Oljoro ili kujiweka imara
zaidi kwa kuwa tumeweka mkakati msimu ujao lazima tuwe tumepanda ligi
daraja la Kwanza (FDL)” alisema Mwaimu.
AFC
imesajili wachezaji 20 na kufanya timu hiyo kuwa na sura ya wachezaji
wapya kulinganisha na msimu uliopita ili kuongeza ushindani wa tofauti
na msimu uliopita ambapo AFC haikufanikisha malengo yake ya kulejea FDL.
“Kikosi
cha mwaka huu ni cha kipekee kuna wachezaji kutoka Morogoro, Tanga ,
Dar es Salaam, Zanzibar na wazawa kutoka hapa hapa Arusha hivyo Kutokana
na mchanganyiko huo kila mchezaji akipata nafasi ya kucheza basi
atahakikisha anamfurahisha Mwalimu hivyo tutakuwa na wachezaji wenye
ushindani” alisema Mwaimu.
Mwaimu
aliongeza kuwa wapo kwenye mazungumzo na Kocha maarufu Tanzania ili
akinoe kikosi cha AFC huku wakitegemea mwishoni mwa wiki hii kukamilisha
taratibu zote za kumpata Kocha huyo ambaye hakumtaja jina lake, huku
akisema kwa sasa timu hiyo ipo chini ya Ally Wingi ambaye ni mwalimu wa
magolikipa.
Ratiba
ya SDL inaonesha ligi hiyo inaanza kutimua vumbi Septemba 14, japo
msimu uliopita ilipangwa hivyo na hatimaye haikuwezekana hadi Disemba
ligi hiyo ilipoanza.
Sambamba
na hilo ratiba inaonesha dirisha dogo la ushajili linafunguliwa
Septemba 15, jambo ambalo linaashiria kuwa gumu kwa TFF kufanikiwa
kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja.
AFC
katika SDL imepangwa kundi B ikwa pamoja na Alliance FC ya Mwanza,
Madini FCya Arusha, Bulyanhulu FC ya Shinyanga, JKT Rwankome ya Mara ,
na Pamba ya Mwanza.
Post a Comment