NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
zaidi ya
wanariadha 100 wamejitokeza kushiriki mashindano ya Mount Meru Marathoni
yaliyofanjika mwishoni mwa wiki jijini hapa ambayo yalianza eneo na Crock Tower na kumalizika
katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
mbio za
Mount Meru zinafanyika kwa mara baada ya kusimama kwa muda wa miaka 15 kwa
kukosa udhamini, hivyo chama cha riadha mkoa wa Arusha ikishirikiana na chama
cha Riadha Taifa (RT) Wameamua kurejesha mashindano hayo kwa mara nyingine.
mratibu wa
mashindano hayo Fredy Nikolas alisema kuwa lengo la mashindanio hayo ni
kuimalisha mchezo huo huku akihaidi mwakani kuimarisha zaidi hasa kwa washindi
ili waweze kupata fulsa ya kushiriki ashindano mbalimbali ya kitaifa na
kimataifa.
mashindano
hayo yaligawanywa katika makundi mawili, mbio za km 5 na mbio za km 21, kwa
upande wa mbio za km 5 kwa upande wa wanaume Denis Malley alifanikiwa
kuwamshindi baada ya kutumia muda wa dakika 23:3813, wa pili ni Joseph Siima
26:51:85, wengine ni Maxmilian Irang 30:06:45 na Hassan Ankway 33:08:45
kwa wanawake
KM 5 Mary Naali aliyetumia dakika 20:52:00, wengine ni Silvia Joseph 26:26:00 na
Victoria Thmas 42:04:52.
wakati kwa
wanaume waliokimbia Km 21 Marko Silvester Alifanikiwa kuwa mshindi kwa kutumia
saa 1:02:37akifuatiwa a Faraja Laizer 1:02:53 na joseph Sule aliweza kushika nafasi
ya tatu kwa kutumia muda wa saa 1:03:11.
na kwa
upande wa wanawake mbio za KM 21 Angelina Tserealiweza kuwa mshindi baada ya
kumaliza kwa kutumia saa 1:14:05 akifuatiwa na RozaliaFabia 1:18:15 na Rebeka
Kavina alimaliza kwa muda wa saa 1:20:00
mshindi wa kwanza katika mbio za Km 21 amejinyakulia
kiasi sh 200,000/=, medali na tisheti maalumu, huku wale wa Km 5 wakiambulia
medali na tisheti ikiwa kama pongezi kwa kushiriki mashindano hayo.
Post a Comment